RC DANIEL CHONGOLO AZINDUA AWAMU YA PILI YA BODI YA PAROLE YA MKOA WA SONGWE
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mheshimiwa Daniel Chongolo, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Parole baada ya kuizindua bodi hiyo Septemba 17, 2024.
...............................
Na Mwandishi Wetu, Songwe.
MKUU wa Mkoa wa Songwe, Mheshimiwa Daniel Chongolo, amezindua rasmi awamu
ya pili ya Bodi ya Parole ya mkoa wa Songwe. Uzinduzi huo umefanyika baada ya
muda wa bodi ya awali kumalizika mwaka 2023, ambapo bodi hiyo hudumu kwa
kipindi cha miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake hadi kuundwa kwa bodi mpya.
Hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo Imefanyika jana katika ukumbi wa Mpende,
jirani na Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, na imehudhuriwa na RPO SACP John F
Daud kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la magereza pamoja na wadau
mbalimbali wa sekta ya sheria na urekebishaji wa wafungwa. Bodi hiyo inalengo
la kuwasaidia wafungwa ambao wanakidhi vigezo vya kutumikia kifungo cha nje ya
gereza, hatua inayolenga kusaidia kuwarudisha wafungwa hao kwenye jamii kwa
taratibu za kisheria.
Aidha Mhe. Chongolo amepongeza juhudi za bodi katika kuhakikisha haki
inatendeka kwa wafungwa wanaostahili, na amesisitiza umuhimu wa bodi hiyo
katika kuboresha utekelezaji wa majukumu ya bodi . Bodi mpya inatarajiwa
kuendeleza mchakato wa kupunguza msongamano gerezani kwa kuwaruhusu wafungwa
wenye sifa kutumikia vifungo vya nje chini ya uangalizi maalum.
Bodi hiyo inatarajiwa kuleta ufanisi zaidi katika utekelezaji wa majukumu
ya Bodi ya Parole kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
No comments