Breaking News

KATIBU CCM MKOA WA PWANI: MSIWAPOTEZE VIONGOZI WAZURI KWA SABABU YA CHUKI ZENU ZA MAJUMBANI

Mkutano wa ndani ukifanyika

..............................

Na Mwandishi Wetu 

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani  wameaswa kutowapoteza viongozi wazuri katika mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa kutokana na chuki zao binafsi.

Hayo yamesemwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani, Kitte Adam Mfilinge wakati alipokuwa akiongea katika Mkutano wa ndani na viongozi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mabaraza ya Jumuiya za CCM  na wazee maarufu uliofanyika leo tarehe 18/09/2024 katika ukumbi wa Pentagon ulioko Mlandizi Wilaya ya Kibaha Vijijini.

 Kitte amesema wako viongozi ambao wanagombana majumbani kisha wanatumia nafasi  hiyo kuleta magonvi kwenye vikao na kukata majina ya watu ambao wangefaa kuwa Viongozi.

" Msiwapoteze viongozi wazuri kwa sababu ya chuki zenu za majumbani" Kitte

Amesema unapofika wakati  wa uchaguzi kila mmoja anatakiwa acheze mechi zake kutokana na nafasi walizo nazo.

 Kitte amesema " Ukiwa Kiongozi jipime kwa kutatua matatizo ya watu unaowaongoza ndipo uwezo wako utakupa tena nafasi ya kuongozi."

Aidha amewataka viongozi hao kwenda katika maeneo yao na kuwaunganisha Wanaccm ili kulinda umoja na heshima ya CCM.

Amemalizia kwa kuendelea kumpongeza Mhe, Daktari Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na kasi ya maendeleo anayoileta katika Taifa la Tanzania.

Mkutano ukiendelea
Viongozi wakiwa meza kuu
Mkutano ukiendelea
 

No comments