Breaking News

MBUNGE MAVUNDE AZINDUA UJENZI JENGO LA MAPUMZIKO HOSPITALI YA MKOA WA DODOMA

MBUNGE wa Jimbo la Dodoma mjini, Mh. Anthony Mavunde amezindua ujenzi wa jengo la mapumziko la wananchi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kusema kuwa ujenzi huo ni sehemu ya utatuzi wa changamoto zinzazowakabili wananchi.

Alisema kuwa nje ya jengo hilo kuna eneo ambalo wanakaa wananchi ambao asilimia kubwa hawaishi katika Jiji la Dodoma na wanatumia sehemu ile kama sehemu ya kupumzikia kwaajili ya kusubiri muda wa kuwaona wagonjwa wao.

Aliongeza kuwa wapo baadhi ambao hawana sehemu ya kulala na hawana makazi Dodoma na hawawezi kurudi walipotoka kwasababu ya umbali na gharama za usafiri.

Kuna wakati mwingine wakina mama, baba na watoto wanachanganyikana na kulala sehemu moja.

Kulingana na maadili ya kitanzania sio vema sana kuchanganyika watu wa jinsi tofauti sehemu moja na hasa ambao kwa namna moja au nyingine hawana uhusiano wowote. jambo hili lilinigusa sana nikasema moja ya sadaka, Mungu akinijalia na nitapenda niiache kama alama ni kuwahifadhi na kuwasitiri wananchi wangu ambao wanakaa katika eneo lile ambalo lipo wazi.

Nikasema nitalifanyia kazi na leo ndugu zangu nimezindua rasmi ujenzi wa jengo la kisasa kabisa na wananchi wa ndani na nje ya Dodoma watapata sehemu nzuri ya kupumzika" alisema Mavunde.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dkt. Sarah Ludovick alitoa taarifa fupi kuhusu hospitali hiyo na kueleza changamoto wanazopitia katika baadhi ya majengo yanayotoa huduma hospitalini hapo.

Alisema kuwa hospitali hiyo ina miaka 104 na ilianza kama kituo cha afya na imekua na kufikia hadhi ya kuwa hospitali ya Mkoa.

Aliongeza kuwa hospitali inatoa huduma kwakupitia sera, miongozo na taratibu zilizowekwa na Wizara ya Afya na kutumia fursa hiyo kumshukuru Mbunge Mavunde kwa moyo wake wa kutatua moja ya changamoto iliyokuwa inawakabili wananchi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya Cde Charles Mamba amepoingeza hatua hii kubwa ya ujenzi wa jengo la kupumzikia wananchi na kusema kuwa CCM inaunga mkono jitihada zinazofanywa na Mbunge Mavunde katika kuhudumia wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Dodoma Legends Ndg. Ahmad Toufiq amesema wamefurahishwa na kazi kubwa anayoifanya Mbunge Mavunde hivyo na wao kuchangia mifuko 100 ya saruji kuunga mkono hatua hizi.




 

No comments