DIWANI MTANGA APITA NYUMBA KWA NYUMBA KUHAMASISHA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA
Diwani wa Kata ya Ngamiani Kusini, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mtanga Aweso (kushoto), akiwa na wajumbe wa kamati yake kuhamasishaji Wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura.
................................
Na Mashaka Kibaya, Tanga.
WAKAZI wa Ngamiani Kusini Jijini Tanga,wametakiwa kuona umuhimu wa
kujiandikisha kwenye daktari la kudumu la wapiga kura, ili kupata haki ya
kuchagua Viongozi wao kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika
Novemba 27 Mwaka huu.
Diwani wa Kata ya Ngamiani Kusini, Mtanga Aweso, Jana akiwa na Kamati yake
kufanya uhamasishaji Wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga
kura, akisema kuwa uhamasishaji huo ni kupitia utaratibu wa nyumba kwa nyumba.
Akiwa katika eneo la Mitaa ya barabara 17 Jijini Tanga, Diwani Mtanga
alisema, tayari zoezi la uandikishaji limeanza, hivyo na wao kupitia nafasi zao
wanao wajibu wa kuendelea kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kujiandikisha kwenye
daktari la kudumu.
Amesema kwamba, wananchi watakapochukua hatua ya kujiandikisha ndipo
watakapopata fursa ya kuchagua Viongozi wao hatua ambayo itawasaidia katika
kuharakisha maendeleo yao.
Licha ya Diwani Mwatanga kufanya hamasa juu ya Wananchi kujiandikisha
kwenye daktari la kudumu la wapiga kura lakini pia alitumia fursa hiyo
kuhamasisha Vijana kujiunga katika Vikundi ili kunufaika na mikopo ya Vijana,
Wanawake na Walemavu.
Diwani huyo alisema kwamba, dirisha la utolewaji mikopo hiyo
limeshafunguliwa na kuwa walengwa wanatakiwa kwenda kwenye Ofisi za Watendaji
Kata ili kuweza kupewa miongozo juu ya namna wanavyoweza kunufaika na Mikopo
hiyo.
"Kazi yangu ni kuelimisha wananchi, Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu
Hassan imeanza kutoa mikopo...dirisha limeshafunguliwa hivyo vijana, wanawake
na walemavu wajiunge katika vikundi ili kuweza kunufaika na mikopo ya asilimia
kumi" alisema Diwani Mwatanga Aweso.
Katika ziara hiyo Diwani huyo aliambatana na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi
CCM Kata hiyo ya Ngamiani Kusini, Masika Mwinshehe, ambaye mbali na kuhamasisha
zoezi la Wananchi kujiandikisha kwenye daktari la kudumu pia aliwakbusha
wanaCCM kuwa na Kadi za Kilelektroniksi.
"Ziara yetu hii lengo lake ni kuhamasisha wananchi kujiandikisha
kwenye daktari la kudumu la wapiga kura, kama Chama pia tunatazama utekelezaji
Ilani na kuhimiza uhai na ndio maana nakumbusha kadi za
Kilelektroniksi"alisema Katibu CCM Kata,Masika Mwinshehe.
Aidha Masika amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, Ummy Mwalimu, kwa
kuwezesha upatikanaji wa Simu ya nyongeza ili kufanikisha utaratibu wa wanaCCM
kuingia kwenye mfumo wa Kilelektroniksi.
Diwani wa Kata ya Ngamiani Kusini, Mtanga Aweso (katikati), akiwa na wajumbe wa kamati yake ya uhamasishaji watu kwenda kujiandikisha kwenye dafati hilo.
Diwani wa Kata ya Ngamiani Kusini, Mtanga Aweso (kushoto), na mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo wakionesha furaha wakati wa zoezi la uhamasishaji.
No comments