RAIS SAMIA AZINDUA ZOEZI LA UANDIKISHAJI KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

Zoezi hili la siku 10 limeanza leo Tarehe 11 hadi 20 Octoba 2024. Tukumbuke Kauli Mbiu ya uchaguzi huu ni Serikali za Mitaa ni Sauti ya Wananchi. Hivyo Rais Samia anawahimiza Watanzania wote wenye sifa za kuchagua na kuchaguliwa kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha ili waweze kushiriki Uchaguzi huu muhimu Tarehe 27.11.2024.
No comments