TET NA TEZ ZA SAINI MKATABA WA KUSHIRIKIANA KIUTENDAJI
Mkurgenzi Mkuu wa Taasisi ya E;limu Tanzani (TET) Dkt. Aneth Komba (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Zanzibar (TEZ) ,Bw.Abdallah Mohamed Musa wakionesha hati za makubaliano ya ushirikiano huo baada ya kuusaini Oktoba 11, 202 huku tukio hilo likishuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ,Zanzibar Bw. Khalid Masoud Waziri.
.....................................
Na Mwandishi Wetu.
TAASISI ya Elimu Tanzaia (TET) na Taasisi ya Elimu Zanzibar(TEZ) leo tarehe
11/10/2024 zimesaini hati mbili za makubaliano ya kiutendaji kwenye eneo la
vifaa vya kufundishia na kujifunzia ambapo lengo kuu ni kuweka ushirikiano kwa
pande zote mbili katika kukuza suala la elimu .
Makubaliano hayo yamesainiwa na wakurugenzi wakuu wa Taasisi hizo ambapo
kwa upande wa TET , aliyesaini alikuwa Mkurugenzi Mkuu Dkt. Aneth Komba na
upande wa TEZ makubaliano yamesainiwa na Mkurugenzi Mkuu ,Bw.Abdallah Mohamed
Musa.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ,Zanzibar Bw. Khalid
Masoud Waziri ambaye alikuwa shuhuda katika hafla hiyo ya utiaji Saini
,amezitaka pande zote mbili kufanya ushirikiano mzuri wenye lengo la kuinua
elimu katika maeneo yote.
“Hili ni jambo kubwa na jema lenye lengo la kuinua elimu katika maeneo
yetu, hivyo naomba mshirikiane vizuri mbadilishane wataalamu katika kuhakikisha
makubaliano mliyoyafikia yanaleta tija katika suala la elimu”amesema Bw.Waziri.
Kwa upande wake ,Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba amesema kuwa hati
ya kwanza ni ya ushirikiano katika uchapaji wa vitabu vya Elimu ya Sekondari
vilivyoandaliwa kwa kufuata mtaala ulioboreshwa wa 2023 na lengo kuu likiwa ni
kuongeza ushiriki wa pande zote mbili katika kuchapa na kusambaza vitabu vya
elimu ya sekondari kwa wakati ili viweze kupatikana katika pande zote za nchi
kabla ya muda wa utekelezaji wa mtaala kuanza kwa vidato husika.
Aidha, Dkt. Komba ameeleza kuwa hati ya pili inahusu uandishi wa vitabu vya
elimu ngazi ya Maandalizi na Elimu ya Msingi ambapo ,ushirikiano huo unalenga
kuunganisha nguvu kazi, utaalamu na uzoefu ili kuandaa vitabu vyenye ubora
unaostahili kwaajili ya wanafunzi wetu wa ngazi hiyo ya elimu.
“Ni matumaini yangu kuwa ushirikiano huu utaongeza tija zaidi katika utoaji
wa elimu iliyo bora katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”amesema Dkt. Komba.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TEZ , Bw.Abdallah Mohamed Mussa amesema
kuwa ushirikiano huo utawezesha katika ukuaaji wa limu Zanzibara kutokana na
makubaliano hayo .
“Hakika huu ni ushirkkiano bora wenye lengo jema kwenye elimu kwa pande
zote mbilli na kuwa tutahakikisha tunafanya kazi kwa weledi na kubadilishana
uzoefu katika kufanya kazi zote zilizopo kwenye makubalino hayo”amesema, Bw.
Musa.
Mkurgenzi Mkuu wa Taasisi ya E;limu Tanzani (TET) Dkt. Aneth Komba (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Zanzibar (TEZ) ,Bw.Abdallah Mohamed Musa wakibadilishana hati hizo baada ya kuzisaini.
Viongozi hao wakisaini hati hizo. Anayeshuhudia katikati ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ,Zanzibar Bw. Khalid Masoud Waziri.
Mkuu wa Taasisi ya Elimu Zanzibar (TEZ) ,Bw.Abdallah Mohamed Musa, akizungumza.
Mkurgenzi Mkuu wa Taasisi ya E;limu Tanzani (TET) Dkt. Aneth Komba akizungumza baada ya kuingia makubaliano hayo.
Wadau wakiwa kwenye tukio la makubaliano hayo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ,Zanzibar Bw. Khalid Masoud Waziri, akizungumza kwenye hafla hiyo.
No comments