TEA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA KITAIFA YA JUMA LA ELIMU YA WATU WAZIMA TABORA, RAIS SAMIA ATAJWA
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Bestina Magutu akitoa maelezo kwa Wanafunzi na wadau mbalimbali waliotembelea banda la mamlaka hiyo kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Juma la Elimu ya Watu Wazima yanayoendelea katika Viwanja vya Chipukizi mkoani Tabora ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
..............................
Na Mwandishi Wetu,
Tabora
MAMLAKA ya Elimu
Tanzania (TEA), ambayo ni Taasisi ya Serikali chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia imeshiriki Maadhimisho ya Kitaifa ya Juma la
Elimu ya Watu Wazima yanayoendelea katika Viwanja vya Chipukizi mkoani Tabora .
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Bestina
Magutu, akizungumza katika maadhimisho hayo alisema maadhimisho hayo yanatoa
fursa nzuri kwa jamii kuelewa umuhimu wa elimu ya watu wazima na jinsi TEA
inavyochangia katika maendeleo ya elimu nchini.
Alisema
majukumu ya TEA kupitia mfuko wa elimu wa Taifa imekuwa ikiboresha mazingira
bora ya kujifunzia na kufundishia na kuboresha miundombinu ya elimu kama
madarasa na mingine yote.
Magutu
alisema katika ushiriki wa maadhimisho hayo wamekutana na wadau mbalimbali na
kuweza kubadilishana uzoefu wa namna ya kuongeza ufanisi wa uboreshaji wa
miundombinu ya elimu na namna ya
kuitunza ikizingatiwa kuwa Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa kazi hiyo.
“Maadhimisho
haya yanatoa fursa nzuri
kwa jamii kuelewa umuhimu wa elimu ya watu wazima na jinsi TEA inavyochangia
katika maendeleo ya elimu nchini na ndio maana tumeyahimiza makundi mbalimbali
ya watu kuja kushiriki,” alisema Magutu.
Alisema maadhimisho hayo yanatoa fursa nzuri kwa jamii kuelewa umuhimu wa elimu ya watu wazima ambayo licha ya wahusika kuwa na umri mkubwa kupitia elimu hiyo imewaongezea maarifa na kupiga hatua kimaisha kwani baadhi yao walikuwa wamekatisha masomo yao kwa sababu mbalimbali.
Katika maadhimisho hayo wanafunzi na wadau wengine mbalimbali wamekuwa
wakifika banda la mamlaka hiyo ili
kuongeza uelewa juu ya utendaji kazi wake ambapo
baadhi yao wamepongeza jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za
kuboresha miundombinu ya elimu nchini.Afisa Miradi wa TEA, Lusungu Kaduma (kulia) akitoa maelezo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo kwenye maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Bi. Eva Shumbusho na katikati ni Afisa Utafutaji Rasilimali, Bi Joyce Minja.
Elimu ikiendelea kutolewa kwenye maadhimisho hayo.
Taswira ya maadhimisho hayo.
No comments