DKT.MPANGO AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI TABORA
........................................
Na Mwandishi Wetu, Tabora
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor
Mpango ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha miundombinu ya vyanzo vya maji vinatunzwa ili idumu kwa muda mrefu.
Dkt.Mpango ametoa rai hiyo kwenye
Hafla ya uwekaji jiwe la msingi la mradi
wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika miji ya Sikonge, Urambo na Kaliua
wenye thamani ya shilingi Bilioni 143.26 iliyofanyika katika mji wa Sikonge
Mkoani Tabora.
Dkt.Mpango ameishukuru serikali ya India kwa ushirikiano mzuri ambao
umewezesha kufanikisha maendeleo kwa serikali za Tanzania na India.
Awali akizungumzia mradi huo Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew
(Mb) amesema mradi huo ni sehemu ya mradi wa maji wa miji 28 ambao unatekelezwa
kupitia mkopo wenye masharti nafuu kutoka Serikali ya India.
Mhandisi Kundo ameishukuru Serikali
kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji nchini.
Pia, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amesema mradi
huo ulianza kutekelezwa Aprili 2023 na utakamilika Oktoba 2025.
Mhandisi Mwajuma amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa Wizara itaendelea
kusimamia kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.
Amesema mradi huo utazalisha lita miliomi 24.76 kwa siku na kuhudumia zaidi ya wakazi 490,926 waliopo katika miji ya Sikonge, Urambo, Kaliua na Uyui pamoja na vijiji 63 ambapo ameeleza kuwa Ultekelezaji wa mradi huo umefika asilimia 48.
Taswira ya uzinduzi wa mradi huo.
Viongozi mbalimbali wakimsikiliza Dkt. Mpango (hayupo pichani)
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akipokea taarifa ya mradi huo.
No comments