MWENYEKITI CCM MWANZA AWASHUKURU WANA MWANZA KWA MAPOKEZI MAKUBWA YA RAIS SAMIA
..........................
Na Dotto Mwaibale
MWENYEKITI wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Ndugu Michael Masanja Smart amewashukuru
Wananchi wa mkoa huo kwa mapokezi makubwa waliyoyafanya ya kumpokea Rais Dkt.
Samia Suluhu Hassan alipowasili leo Oktoba 12, 2024 kwa ziara ya kikazi.
“ Moyo wangu
umejawa shukrani kwa wana Mwanza jinsi walivyojitokeza kwa wingi kwenye
mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuja kwa ziara ya kikazi na
atakuwepo kwenye mkoa wetu hadi Oktoba 15,2024,” alisema Smart.
Smart alitumia nafasi hiyo kuwaomba wana Mwanza kwa mara nyingine tena wajitokeze kwa wingi Oktoba 14, 2024 kwenye Kilele Cha Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Uwanja wa CCM Kirumba Wilaya ya Ilemela.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na viongozi na wazee wa Mkoa wa Mwanza mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi.
Wananchi wa Mkoa wa Mwanza walivyojitokeza katika mapokezi ya mpendwa Rais wao Dkt. Samia Suluhu Hassan Pansiansi mkoani Mwanza.
Wananchi wa Mwanza wakiwa kwenye mapokezi hayo.
Taswira ya mapokezi hayo.
Mapokezi yakiendelea.
Wana Mwanza wakionesha furaha yao wakati wa mapokezi hayo.
Vijana wa UVCCM wakionesha furaha zao wakati wa mapokezi hayo.
No comments