RC LINDI AWATAKA WANAWAKE KUWA NA MAAMUZI YASIYO LEGALEGA
…………………………………
Na Mwandishi Wetu, Lindi
MKUU wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack ametoa wito kwa wanawake wa Mkoa wa
Lindi kuwa na maamuzi na ujasiri Mkubwa katika kuyafikia malengo bila kugeuka
nyuma.
Mhe. Telack ametoa wito huo katika hafla iliyoandaliwa na wome's Gala 2024
yenye lengo la kuwakutanisha wanawake wakada tofauti tofauti kubadilishana
uzoefu na kupata elimu mbalimbali zitakazowezesha kuwaongezea maarifa katika
nyanja za kiuchumi, kijamii , kiutamaduni na kisiasa.
"Sasa akina mama ili tuweze kufika huko, kufikia malengo ambayo
tunataka kuyafikia , tunachotakiwa kuwa nacho ni ujasiri mkubwa , kuwa na
maamuzi ambayo hayalegilegi kwenye yale ambayo unataka kwenda kuyafikia,
usikatishwe tamaa na yoyote wakati unataka kwenda mbele kama lile unalofikiria
unataka kwenda nalo unauhakika utatoboa na utafika unakotaka kwenda .
Amesema hatua hiyo ya kuchukua maamuzi yanatoka na changamoto nyingi ambazo
mwanamke anakutana nazo.
No comments