DC KUBECHA: MALEZI YA MTOTO SI YA BABA NA MAMA PEKE YAO NI YA JAMII NZIMA
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Japhari Kubecha (katikati( alipokuwa akishiriki Mahafali ya darasa la saba katika Shule ya Mwambani English Medium iliyopo jijini Tanga.
.............................
Na Mwandishi Wetu, Tanga
MKUU wa Wilaya ya Tanga, Japhari Kubecha amesema malezi kwa watoto si jukumu la la baba na mama peke yao bali ni la jamii nzima kwa ujumla.
Kubecha ambaye alikuwa mgeni rasmi ameyasema hayo kwenye Mahafali ya Darasa la Saba katika Shule ya Mwambani English Medium iliyopo nje kidogo ya jiji la Tanga.
"Malezi ya watoto si jukumu la baba na mama waliowazaa watoto hao bali ni la jamii nzima inayowazunguka," alisema Kubecha.
Katika hatua nyingine Kubecha aliwataka wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuwalinda watoto hao na kuacha kuwafanyia vitendo vya kikatili ambavyo ni kosa kisheria ambapo alihimiza kuwalinda watoto hao ili waweze kutimiza ndoto zao.
Aidha, Kubecha alipata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali yaliondaliwa na Wanafunzi na kujionea mafunzo ya vitendo yaliyohusisha Upishi ,Jinsi ya Kukabili majanga ya Moto kwa Teknolojia ya kisasa na kupata Historia a nchi yetu pamoja na viongozi wake.
Mwanafunzi akionesha mafunzo kwa vitendo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Japhari Kubecha.
Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo akielezea Historia ya nchi yetu na viongozi wake.
DC Kubecha na viongozi wengine wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mwanafunzi akifanya mafunzo kwa vitendo mbele ya mkuu wa wilaya.
Mafunzo kwa vitendo yakiendelea.
Wazazi na viongozi wakiwa kwenye mahafali hayo.
No comments