Breaking News

WAFANYAKAZI KAMPUNI ZA DNATA, EMIRATES LEISURE RETAIL ZANZIBAR WAFANYA USAFI UFUKWE WA KILIMANI

Meneja Oparesheni wa Kampuni ya Emirates Leisure Retail Zanzibar, Sasikumar Venkatachalam (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo na wa Kampuni za DNATA wakati walipokuwa wakifanya usafi katika Ufukwe wa Kilimani Zanzibar.

................................

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

WAFANYAKAZI wa Kampuni za DNATA na Emirates Leisure Retail Zanzibar zinazojishughulisha na utoaji huduma kwa wageni katika Uwanja mpya wa Ndege Zanzibar (AAKIA) ,wamejitolea kufanya usafi katika Ufukwe wa Kilimani Zanzibar.

Meneja Oparesheni wa Kampuni ya Emirates Leisure Retail Zanzibar, Sasikumar Venkatachalam akizungumza wakati wa tukio hilo alisema katika kuunga mkono jitihada za Serikali za utunzaji wa mazingira kampuni hizo ziliamua kuandaa siku kwa ajili ya kufanya usafi katika uwanja huo.

“ Pamoja na kutoa huduma kwa wageni katika uwanja huu pia ni wajibu wetu kuhakikisha mazingira tunayotolea huduma yanakuwa ni masafi na ndio maana tupo hapa tukifanya usafi,” alisema Venkatachalam.

Alisema kuwa kampuni hizo zimeanzisha utaratibu wa kujitolea kwa jamii kufanya usafi ili kutunza mazingira yote wanayoizunguka jamii hasa maeneo ya fukwe.

Venkatachalam alisema kazi hiyo ya kufanya usafi itakuwa ni endelevu ambapo pia watafanya utaratibu wa kuhamasisha jamii kushiriki kwenye kazi hiyo ambayo ni muhimu katika utunzaji wa mazingira. 

Usafi ukifanyika
Usafi ukiendelea kufanyika
Meneja Mkazi wa Kampuni ya Emirates leisure Retail Zanzibar, Paul Charbel Atallah akishiriki kufanya usafi na mtoto wake.
Usafi ukiendelea
Meneja Mkazi wa Kampuni ya Emirates Leisure Retail Zanzibar, Paul Charbel Atallah akishiriki kufanya usafi.
 

No comments