DCEA YAKAMATA KILO 2, 207 ZA DAWA ZA KULEVYA WATUHUMIWA SABA WATIWA MBARONI
Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, akitoa taarifa ya tukio hilo kwa waandishi wa habari Novemba 25,2024 jijini Dar es Salaam.
................................
Na Mwandishi Wetu/ Dar es Salaam
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi imekamata jumla ya kilo 2,207.56 za dawa sa kulevya na dawa tiba zenye asili ya kulevya katika mikoa ya Tanga na Dar es Salaam na watuhumiwa saba wanashikiliwa kwa kuhusishwa na dawa hizo.
Kati ya dawa hizo ambazo zimekamatwa Skanka ni
kilo 1,500.6 ,methamphetamine kilo 687.76 ,heroin kilo 19.20 na chupa 10 za
dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya Fentanyl.
Akizungumza Novemba jijini Dar es Salaam
, Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya
(DCEA), Aretas Lyimo amesema katika Novemba 14 mwaka huu katika Wilaya ya
Kigamboni Mtaa wa Nyangwale wamemawakamata watuhumiwa Mohamed Bakari(40) na
Sullesh Mhailoh( 36) ambao ni wakazi wa Mabibo wamakamatwa wakiwa na kilo
1350.4 za dawa za kulevya aina ya Skanka.
Amesema dawa hizo zilikuwa zimefichwa ndani ya
nyumba aliyopanga mtuhumiwa Mohamed ambayo aliitumia kama ghala la kuhifadhi
dawa hizo .Pia dawa nyingine zilipatikana ndani ya gari aina ya Nissan Juke
yenye namba za usajili T 534 EJC zikiwa tayari kwa kusambazwa.
Kamishina Lyimo amesema pia tarehe hiyo hiyo
katika Mtaa wa Pweza Sinza E wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam mtuhumiwa
Iddy Mohamed Iddy (46) mkazi wa Chanika Buyuni alikamatwa akiwa na kilo 150.2 za
Skanka zilizokuwa zimefichwa katika maboksi ya sabuni.
Pia amesema na baadhi ya dawa hizo nyingine
zilikuwa zimefichwa kwenye boksi lililotengenezwa kwa bati gumu na kupachikwa
katika chassis ya gari aina ya Scania lenye namba za usajili wa Afrika Kusini
LN87XGP. Gari hiyo imekuwa ikitumika kusafirisha bidhaa mbalimbali kutoka nje
ya nchi.
Akielezea zaidi amesema Novemba 17 mwaka huu
katika Jiji la Tanga watuhumiwa Ally Kassim Ally (52) na Fahad Ally Kassim (36)
walikamatwa Mtaa wa Mwakibila wakiwa na kilo 706.96 za dawa za kulevya aina ya
heroin na methamphetamine.
Kamishina Jenerali Lyimo amesema baadhi ya dawa
hizo zimepatikana ndani ya gari aina ya Toyota Noah yenye namba za usajili T
714 EGX huku nyingine zikibainika kufichwa katika nyumba aliyopanga mtuhumiwa.
Pia amesema Novemba 19 mwaka huu katika Mtaa wa
Kipati na Nyamwezi Kariakoo jijini Dar es Salaam watuhumiwa Michael
Mziwanda (28) mkazi Tabata Segerea na Tumpale Mwasakila (32) Mkazi wa Temeke
Mikoroshini walikamatwa na chupa 10 za dawa zenye asili ya kulevya aina ya
Fentanyl wakiwa nazo katika duka la M-Pesa .
Aidha katika opresheni hizo zilizofanyika
wamekamata magari matatu na boti moja ambavyo vimekuwa vikitumika katika
uhalifu na viko chini ya ulinzi.
"Dawa zilizokamatwa ni nyingi na zingeweza
kuwa na madhara makubwa kwa jamii na Taifa ikiwa zingeingia mitaani. Dawa hizi
haziathiri tu wale waliokwishaanza matumizi ya dawa za kulevya bali pia
wafanyabiashara hawa wa dawa hulenga watu wengine ambao hajaanza matumizi ili
kutanua masoko yao.
Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari.







.jpg)




No comments