RAIS DKT.SAMIA ASISITIZA NCHI ZA SADC KUMALIZA MIGOGORO.
Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali .Mwinyi akihutubia kwa niaba ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan alipomwakilisha kufungua Mkutano wa Viongozi Wakuu na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika uliofanyika jijini Harare Zimbabwe Novemba 20, 2024.
.................................................
Na Mwandishi Wetu, Zimbabwe
Mwenyekiti wa asasi ya siasa, ulinzi na usalama wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia
Suluhu Hassan amezisisitiza nchi za
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC kuunga mkono juhudi za kidiplomasia
za kumaliza Uhasama uliopo baina ya DRC na Rwanda chini ya mchakato wa Angola.
Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali .Mwinyi ameyasema hayo kwa niaba ya Rais Dkt.Samia alipomwakilisha
kufungua Mkutano wa Viongozi Wakuu na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
uliofanyika jijini Harare Zimbabwe tarehe 20 Novemba 2024.
Rais Dk, Samia amefafanua kuwa wakati nchi za SADC zikiendelea kujadili
hali ya Usalama wa Mashariki ya DRC ni vyema kukawekwa mifumo imara ya
Ufuatiliaji na utekelezaji wa maazimio
yanayoidhinishwa na Jumuiya
mbalimbali za Kikanda ikiwemo yale ya
Umoja wa Afrika(AU) na Umoja wa Mataifa (UN).
Ameeleza kuwa hatua hiyo itawezesha kupatikana kwa Misaada ya kifedha na
kilojistik kwa wakati na kuongeza
Ufanisi wa Misheni za SADC na kupunguza
gharama.
Rais Dk, Samia amezishauri nchi za SADC kutumia majadiliano ya Mkutano
huo kutoka na maazimio yatakayokuwa chachu ya kupatikana kwa Amani ya kudumu katika Ukanda
wa SADC na kuwa ni ushahidi wa dhamira ya nchi hizo ya kuleta Amani Endelevu.Viongozi wakiwa kwenye mkutano huo.
No comments