Breaking News

SERIKALI YATOA UTARATIBU UTOAJI MSAADA WA FEDHA KWA WAHANGA WA GHOROFA KARIAKOO

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali nayoendelea katika zoezi la uokoaji ghorofa lililoanguka Kariakoo.

....................................

Na Emmanuel Mbatilo, Dar es Salaam

UTARATIBU wa utoaji wa msaada wa kifedha kwaajili ya kusaidia walioathirika na kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo Jijini Dar es Salaam zitaelekezwa kwenye akaunti maalumu ya maafa 9921159801ambayo ipo BoT na inashughulikiwa na ofisi ya Waziri Mkuu .

Hayo yameelezwa leo Novemba 18, 2024 Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu haki inayoendelea katika zoezi la uokoaji.

Amesema akaunti hiyo ni pekee nchini ambayo inakusanya misaada ya kifedha kwaajhili ya maafa.

"Kuna watu wana nia njema kabisa kwaajili ya kuwasaidia Watanzania, lakini naomba tujizuie kabisa kukusanya michango ya kifedha kutoka kwa mtu yeyote bila kupitia akaunti hii". Amesema Dkt. Yonazi.

Aidha amesema akaunti hiyo ni maalumu imethibitishwa na serikali ili kuweza kuhakikisha misaada inawafikia walengwa na inatimiza malengo ya kutoa misaada hiyo.

Amesema kwasasa operesheni inaendelea mpaka pale watakapokamilisha zoezi la kuokoa baadhi ya watu ambao bado hawajaokolewa.

No comments