ZANZIBAR MPYA CHINI YA RAIS DKT. HUSSEIN ALI MWINYI YAWA NA MAPINDUZI MAKUBWA YA MAENDELEO
............................
Na Dotto Mwaibale
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye ni Rais wa Nane wa Zanzibar amepeleka
Neema nyingi kwa Wanzibar katika kipindi kifupi cha uongozi wake tangu aingie
madarakani.
MAFANIKIO KADHAA YA SERIKALI YAKE KATIKA SEKTA YA
UWEZESHAJI WANANCHI.
Tangu aingie madarakani Rais Dkt. Ali Hussein
Mwinyi Serikali imeweza kutoa mikopo nafuu kwa wananchi 19,906 yenye thamani ya
Sh. 22.5 Bilioni ikiwa ni ongezeko la Sh. 15 Bilioni zilizotolewa awali na
kusababisha ajira kwa wananchi 43,360.
KATIKA ENEO LA ELIMU NA UJASIRIAMALI
Serikali
imeendelea kuendesha mifuko ya Khalifa na ule wa makundi 4.4.2 yaani Vijana
asilimia 4, Wanawake asilimia 4 na Walemavu asilimia 2 kwa kutoa elimu ya
ujasiriamali na mafunzo ya utaalamu wa biashara pamoja na kuwaunganisha na
masoko.
VYAMA 3,666 VIMESAJILIWA
Katika awamu yake hii ya uongozi vyama vya ushirika 3,666 vimesajiliwa vikiendesha shughuli na mitaji. Vyama Mwamvuli vitatu vya maziwa, uvuvi na ushoni vimeimarishwa kwa mafunzo, mitaji na ufuatiliaji wa madeni.
No comments