WAZIRI KOMBO: TANZANIA ITAENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KULETA AMANI
Waziri Mambo ya Nje na Uashirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo akifuatilia Mkutano wa Kawaida wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje (RIMC) wa Nchi Wanachama wa ICGLR uliofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 24 Novemba 2024.
Balozi
wa Tanzania nchini Angola mwenye makazi yake nchini Zambia Mhe. Lt. Gen.
Mathew Edward Mkingule akifuatilia Mkutano wa Kawaida wa 18 wa Mawaziri wa
Mambo ya Nje (RIMC) wa Nchi Wanachama wa ICGLR uliokuwa ukiendelea jijini
Luanda, Angola tarehe 24 Novemba 2024.
Waziri
wa Mambo ya Nje wa Angola Mhe. Balozi Téte António kwenye ufunguzi
wa mkutano wa Kawaida wa 18 wa
Mawaziri wa Mambo ya Nje (RIMC) wa Nchi Wanachama wa ICGLR uliofanyika jijini
Luanda, Angola tarehe 24 Novemba 2024.
Waziri Mambo ya Nje na Uashirikiano wa Afrika
Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo ameeleza kuwa Tanzania ikiwa ni
mwasisi wa Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Mkuu (ICGLR) itaendelea kushirikiana na
nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo na Jumuiya ya Kimataifa katika juhudi za
kutafuta amani ya kudumu kwenye ukanda huo.
Waziri Kombo ameeleza
hayo alipozungumza katika Mkutano wa Kawaida wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje
(RIMC) wa Nchi Wanachama wa ICGLR uliofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 24
Novemba 2024.
Akizungumzia kuhusu
msimamamo, mchango na nafasi ya Tanzania katika kufatua amani na usalama kwenye
ukanda wa Maziwa Makuu Waziri Kombo ameeleza kuwa, Tanzania chini ya uongozi
mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu
Hassan itafanya kazi bila kuchoka kwa kushirikiana na nchi wanachama na Jumuiya
ya Kimataifa kutatua migogoro iliyopo ili kuwa na ukanda wenye amani, ustawi na
ustahimilivu.
“Kama mwanachama
mwanzilishi wa ICGLR, Tanzania inaamini kuwa kuimarika kwa mahusiano ya
kidiplomasia na kuimarishwa kwa utulivu kutaongeza kasi ya maendeleo ya
kiuchumi ya watu wetu katika Ukanda wa Maziwa Makuu” Ameeleza Waziri
Kombo.
Aidha, Waziri Kombo
licha ya kueleza utayari wa Tanzania katika kuendelea kushirikiana na wadau katika
kurejesha amani na usalama kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu, ametoa wito kwa nchi
wanachama kuhakikisha kuwa ushawishi wa washirika wa maendeleo hauathiri
utendaji na ufanisi wa mifumo iliyowekwa ikiwemo Mfumo wa Tahadhari ya Mapema
na Majibu ya Migogoro wa ICGLR (ICGLR Conflict Early Warning and
Response Systems).
Vilevile, amesisitiza
umuhimu wa nchi Wanachama kuheshimu na kutimiza wajibu wake wa kuchangia fedha
kwa Sekretarieti, ikiwa ni ishara ya mshikamano na juhudi za pamoja, katika
kuhakisha Jumuiya inatekeleza mipango na mikakati inayojiwekea ili kufikia
matarajio ya kuwa na ukuanda wenye Usalama, Utulivu, na Maendeleo endelevu.
Pia ametumia fursa hiyo
kuitaka Sekretareti ya ICGLR kuzingatia matumizi mazuri na usimamizi mzuri wa
fedha kwa manufaa ya kanda.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Mhe.
Balozi Téte António akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo ameleeza
ameeleza kuridhishwa kwake na mazungumzo yanayo endelea yakilenga kurejesha uhusiano
wa kidiplomasia kati ya Rwanda na DRC.
Aliendelea kutoa wito
kwa nchi wanachama kwa umoja wao kuendelea kushughulikia changamoto
zinazotishia amani, usalama, na hali ya kibinadamu katika Jamhuri ya Sudan,
Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini, na ghasia zinazoendelea katika
Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Mkutano huo umehudhuriwa na nchi zote 12 Wanachama wa Maziwa Makuu na Mjumbe Maalumu kutoka Umoja wa Mataifa anayesimamia Ukanda wa Maziwa Mkuu Balozi Huang Xia.
No comments