HOSPITALI YA BOMBO YAKIRI MSD KUWA KIMBILIO LA WATEJA
Na Mashaka Kibaya, Tanga
Bohari ya dawa 'Medical Store Department' (MSD) imeelezwa kuwa kimbilio kwenye suala la uwezeshaji wa dawa na vifaa kwa hospitali ya rufaa Bombo Mkoani Tanga, hatua ambayo imesaidua katika kuiwezesha kuendelea kuwahudumia Wananchi kwa ufanisi.
Hayo yamebainika wakati wa Ziara ya Wajumbe ya Bodi ya Bohari ya dawa (MSD) walipotembelea Wateja wao wanaohudumiwa na Kanda ya Tanga, ambapo walipata fursa ya kutembelea hospitali ya rufaa ya Bombo Mkoani Tanga.
Katika taarifa yake kwa Wajumbe hao wa Bodi ya MSD, Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo ya rufaa ambaye pia ni Mganga Mfawidhi Dkt Athumani Kihara alisema, MSD ni kimbilio lao katika upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.
Naye Daktari bingwa wa upasuaji Dkt Rashid ......amepongeza na kuishukuru MSD kwa utoaji huduma nzuri kwa wateja huku Katibu wa hospitali hiyo ya Bombo Dkt Abasi akimshukuru Meneja wa Bohari hiyo ya dawa Kanda ya Tanga kwa jinsi wanavyokuwa wakishirikiana naye katika majukumu ya utendaji wa kazi.
.
Katibu huyo wa hospitali ya rufaa Bombo aliongeza kusema kuwa, licha ya MSD kuwadai fedha nyingi lakini bado wamekuwa wavumilivu huku wakiendelea kuwapatia huduma na hivyo kumudu kuwahudumia Wananchi.
Aidha Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ya Bohari ya dawa Dkt Rukia Mwifunya ambaye pia ni mlezi MSD Kanda ya Tanga, ametoa Rai kwa Uongozi wa hospitali hiyo ya rufaa kuendelea kushirikiana na MSD ili kusaidia kuimarishaji wa afya za Wnanchi na kuwawezesha kuendelea na shughuli zao za kujiletea maendeleo yao.
Elisamehe Macha ni Meneja wa huduma za Sheria wa MSD ambaye licha ya kuonesha kuridhishwa na taarifa kutoka kwa Wateja wao, kwa niaba ya Wajumbe wengine waliombatana alisema kwamba ushauri uliotolewa wanapokea huku akiahidi kufanyika maboresho zaidi.
Katika ziara hiyo ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya MSD kutimiza miaka thelasini ya utendaji kazi wake tangu ilipoundwa, Wajumbe wa bodi wameitumia kufanya tathimini namna ambavyo wanafanya kazi na kufanya maboresho.
No comments