MAGIFTI YA KUGIFTI WIKI YA SABA , YAS WANOGESHA SIKUKUU KWA WATEJA WAO WATOA MAMILIONI
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Kampeni ya Magift ya Kugift inayoendeshwa na Kampuni ya mtandao wa simu za
mkononi wa Yas ikiwa droo ya wiki ya saba wananchi wanaotumia huduma za mtandao
huo wameendelea kuneemeka na kampeni hiyo.
Chiku Rashid mkazi wa jijini Dar, ni miongoni mwa washindi nane walioibuka
na zawadi mbalimbali katika droo ya saba yeye akiondoka na shilingi milioni
moja ambayo amesema itamsaidia kuboresha mtaji wake wa kuuza nguo.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya kiasi hicho, Chiku
amesema zawadi hiyo kwake imekuwa kama ‘sapraiz’ kwani hakuitegemea hivyo
itaboresha biashara yake ya nguo hususan kipindi hiki cha sikukuu ambapo
biashara hiyo ndiyo msimu wake.
“Nawashauri watumiaji wenzangu wa simu kutumia mtandao wa Yas kujipatia
huduma mbalimbali kama vile kununua vocha, vifurushi kufanya miamala kwa
kutumia Mixx by Yas ili nao waweze kuibuka washindi kama mimi.” Alisema Chiku.
Akizungumza baada ya kumkabidhi mshindi huyo mfano wa hundi, Meneja wa
Bidhaa za Yas, Eginga Mohammed amewataka watumiaji wa simu kutumia mtandao wa Yas kwa huduma
mbalimbali kama vile kununua vifurushi, kufanya kwa kutumia Mixx by Yas ili
waweze kuingia kwenye droo na kujishindia zawadi mbalimbali.
Eginga amesema hii ni wiki ya saba kuchezeshwa droo na bado wiki sita na
kuwataka watumiaji wa simu za mkononi kutumia huduma za Yas ili waweze kuibuka
na ushindi ambapo kuna zawadi mbalimbali kama vile, simu janja, pesa taslimu
shilingi milioni moja, milioni tano, milioni kumi pamoja na zawadi ya gari
jipya aina ya Kia Seltos.
Meneja huyo alimalizia kwa kusema wiki ijayo itachezeshwa droo ya nane
ambapo anatarajiwa kupatikana mshindi wa gari hilo jipya na la kisasa aina ya
Kia Seltos.
Meneja wa Bidhaa za Yas, Eginga Mohamed (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi, Chiku Rashid aliyeibuka miongoni mwa washindi wa shilingi milioni moja katika droo ya wiki ya saba wa Kampeni ya Magift ya Kugift. Anayeshuhudia (katikati) ni Meneja wa Wateja Maalum wa Mixx by Yas, Mary Rutta.
No comments