MELI YA MV SERENGETI YAPINDUKA SIKU TATU BAADA YA KUFANYIWA UKAGUZI

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Kampuni ya Meli Tanzania(TASHICO) imetoa taarifa kwa umma kuhusu tukio la
kupinduka kwa meli ya Mv.Serengeti lililotokea usiku wa kuamkia Desemba 26
mwaka huu katika Bandari ya Mwanza Kusini.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni hiyo Paul Sebukoto amesema kuwa Meli hiyo imelalia upande wa nyuma
baada ya maji kuingia ndani.
‘’Meli hii ilikuwa kwenye eneo la Maegesho,Maji yameingia ndani zikiwa
zimepita kama siku mbili au tatu baada ya kufanyiwa ukaguzi uliobaini iko
sawa,kwa hiyo ni lazima kutakuwa na chanzo ambacho kimesababisha maji kuingia
ndani ya meli na kuipeleka chini upande wa nyuma’’alisema Sebukoto na Kuongeza
kuwa
‘’Sasa tofauti na Tafsiri kuwa meli imepinduka au imezama ni kwamba meli
hii haijapinduka wala haijazama isipokuwa tunasema imeegemea upande wa nyuma
baada ya kulemewa na maji yaliyoingia ndani’’
Sebukoto amesema kuwa shughuli zinazofanyika kwa sasa ni kuinyanyua Meli
hiyo kwa nyuma ili iweze kurudi kwenye hali yake ya kawaida na kuondoa yale
maji sanjari na kutafuta chanzo kilichosababisha maji kuingia ya Meli.
‘’Mpaka sasa hatujajua sababu za meli hii kuegemea upande wa nyuma na
kwanini maji yameingia ndani,ni mpaka hapo wataalam watakapoirudisha katika
hali yake ya kawaida ndipo sasa ipandishwe kwenye chelezo kwa ajili ya
kukaguliwa mwili wake wote,hapo ndo tutaweza kutoa taarifa sahihi kuhusu chanzo
’’alisema Sebukoto.
Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tashico amesema kuwa kipaumbele cha
kampuni hiyo ni kuimarisha usalama wa vyombo vyake vinavyotoa huduma ya usafiri
wa abiria na mizigo pamoja na
vilivyoegeshwa kwenye bandari Mwanza kusini.
‘’Changamoto za namna hii zinapojitokeza ni sehemu ya kutufanya sisi
tuzidishe usalama kuliko ilivyokuwa,Tunajali usalama na tunajitahidi kufuata hatua
zote za kiusalama kama inavyotakiwa na sheria za usafirishaji kwa njia ya
maji,Ninachoweza kusema hapa ni kuwa tutazidisha kuweka usalama zaidi ikiwemo
kutumia njia za kisasa kama kufunga kamera pamoja na kuweka mifumo ya kiusalama
ikiwemo alarm.Hizi meli zetu zimetengenezwa zamani,ile mifumo ya kisasa kama
maji yameingia.
No comments