PRADO YAPATA AJALI YAWAKA MOTO YAUA WATU SITA WAKIWEMO WALIMU WANNE RUVUMA
................................
Na Regina Ndumbaro- Ruvuma
Watu sita wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika Wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma.
Ajali hiyo imetokea Desemba 28, 2024, wakati ikisafiri kutoka Kijiji cha Lumalu kilichopo katika Kata ya Upolo kuelekea makao makuu ya wilaya.
Akizungumza kwa njia ya simu, Mkuu wa Wilaya ya
Nyasa, Peres Magiri, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, ambayo imesababisha
vifo vya walimu wanne wa Shule ya Msingi
Lumalu.
Watu wengine waliofariki katika ajali hiyo ni
dereva wa gari hilo Vicent Alel Milinga
na mtu mwingine aliyetajwa kwa jina la
Boniface Mapunda.
Gari lililohusika katika ajali hiyo ni aina ya Prado
lenye namba za usajili T 647 CVR, mali ya Vincent Alel Milinga mkazi wa Kijiji
cha Lumalu, Kata ya Upolo, Wilaya ya Nyasa.
Walimu waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni Damas Damasi Nambombe ,Domenica Abeat Ndau ,Judith Joseph Nyoni na John Silvester Mtuhi.
No comments