YAZID MABALA MHANDISI ANAYEWIWA KUIONA MWIBARA IKIWA KINARA KWA MAENDELEO- BUNDA MKOANI MARA
.........................
UZALENDO ni hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi na
Mzalendo wa kweli wakati wote anaweka maslahi ya nchi na ya jamii mbele.
Uzalendo unabeba dhana
pana ikianzia asili, utamaduni, lugha, siasa, historia zote zikifungwa kwenye
dhana kuu ya utaifa.
Katika Taifa la Tanzania
kumekuwepo na wazalendo wengi, baadhi wamekwisha tangulia mbele za haki akiwemo
aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Julius Kambarage Nyerere, Hayati
Abeid Amani Karume, Hayati Rashid Mfaume Kawawa, Hayati Edward Moringe Sokoine,
Hayati Edward Ngoyai Lowassa, Hayati Bibi Titi Mohamed na wengine wengi.
Leo napenda kumuongelea
Mhandisi Yazid Mabala ambaye ni Mdau wa Maendeleo
aliyejikita kuleta chachu ya mapinduzi ya maendeleo ndani ya Mwibara, Bunda Mkoa wa Mara ni
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayewekeza katika kuwatumikia Wananchi wote
na Watanzania kwa ujumla bila ubaguzi na anaeziishi 4R za Mhe Dkt Samia Suluhu
Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) na Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Taifa kwa Vitendo.
Katika upande
wa utunzaji wa Mazingira nchini, Mhandisi Yazid Mabala ametoa mchango mkubwa wa
Utunzaji wa Mazingira kwa kutoa miche ya miti 5,000 ikiwa ni miche ya miti
mchanganyiko ndani ya Mwibara-Bunda, Mara ili kuhakikisha Tanzania inaendana na
kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kutokana na Sera ya Umoja wa Mataifa ya
utunzaji Mazingira.
Aidha, Mhandisi
Mabala katika kuinua sekta ya Michezo amekuwa mstari wa mbele kuchangia kutokana
na Umuhimu wa Michezo kwenye jamii kwani Michezo inaleta Umoja, Michezo ni
ajira kwa vijana, Michezo ni sehemu ya kujenga afya ya mwili na akili.
Mwaka 2021,
2022, 2023 na Mwaka 2024, Mhandisi Mabala amewezesha Ligi ya mchezo wa mpira wa
miguu ndani ya Mwibara ambapo ametoa vifaa vya michezo ikiwemo Mipira, Jezi,
Maji na Mbuzi kwa ajili ya mshindi wa mashindano ya Michezo yaliyofanywa chini
ya ufadhili wake.
Mwaka 2021 akiwa
kama mdau mpenda maendeleo alipata ombi kutoka Chama Wilaya la kuchangia katika
uandikishaji wa Wanachama wapya ambapo alifanikiwa kuchangia Simu Janja mbili
ili kusaidia Ujenzi wa Chama hicho.
Mwaka 2021 aliwezesha kufanyika kwa kongamano kubwa la
kuwajenga Vijana Kifikra katika kujisimamia Kiuchumi na kuziibua Fursa
zilizojificha za Uzalishaji ili Vijana hao waendelee kujisimamia wao wenyewe
siku zote ndani ya Jimbo la Mwibara na Mgeni Rasmi katika kongamano hilo
alikuwa Joshua Nasari aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda wa Kipindi hicho na
Mbunge wa Jimbo la Mwibara alipewa Mwaliko pia.
Mwaka 2021
alisaidia katika ujenzi wa darasa katika Shule ya Msingi Muungano kwa kuchangia trips za Mchanga na mawe katika ujenzi huo.
Hayo
yaliyotajwa hapo juu ni baadhi ya kazi chache kati ya nyingi ambazo amezifanya
mhandisi huyo kwa ajili ya kusaidia jamii ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwaletea wananchi maendeleo.
Mhandisi Mabala
wakati akitoa salamu za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2025 ameahidi
kuendelea kuisaidia jamii inayomzunguka
ili iendelee kujisimamia katika uzalishaji kwa kuwapa mbinu mbalimbali ili kuweza kukuza pato la mtu mmoja mmoja ili waweze kupiga hatua za maendeleo
kwani hiyo ndiyo furaha yake kuwatumikia wananchi na Watanzania kwa ujumla bila
kujali dini, Kkabila , vyama vyao na jinsia zao.
Binafsi
napenda kuchukua nafasi hii kukutakia mafanikio kwa mipango yako mizuri yenye
lengo ya kuisaidia jamii kwani huo ndio uzalendo wa kweli.
Mhandisi
Mabala Mungu akupe afya njema ili matamanio yako ya kuwaletea wananchi wa Mwibara maendeleo na yakatimie bila ya kusahau kumuomba Mungu kwani kila penye
mafanikio hapakosi changamoto. Kazi Iendelee.
(Makala hii imeandikwa kwa msaada wa ofisi ya Mhandisi Yazid Mabala). kwa mawasiliano ya mwandishi piga namba (0754-362990)
No comments