WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA DKT. STARGOMENA TAX AONGOZA MAZISHI YA MEJA JENERALI BUSUNGU
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Stargomena Lawrence Tax akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa marehemu Meja Jenerali Martine Busungu (Mstaafu) wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo kabla ya mazishi yake yaliyofanyika Kijiji cha Luchelele Jijini Mwanza Disemba 28, 2024.
............................................
Na Mwandishi Wetu, Mwanza.
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Stargomena Lawrence Tax
ameongoza Maafisa, Askari, vijana wa JKT, watumishi wa umma na waombolezaji
katika mazishi ya marehemu Meja Jenerali
Martine Busungu (Mstaafu) yaliyofanyika Kijiji cha Luchelele Jijini Mwanza
tarehe 28 Disemba 2024.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob
John Mkunda katika mazishi hayo, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa
Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajab Nduku Mabere amesema, Meja Jenerali Busungu
(Mstaafu) akiwa mtumishi ndani ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
amelitumikia jeshi kwa kipindi cha miaka thelathini na nne (34), ambapo alikuwa
mwaminifu, mtiifu Hodari katika kutekeleza majukumu yake.
Meja Jenerali Busungu Mstaafu) alifariki dunia tarehe 24 Disemba 2024
katika hospitali ya taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Stargomena Lawrence Tax akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Meja Jenerali Mstaafu Busungu.
Heshima za mwisho zikitolewa kwa marehemu.
Watoto wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao.
Maafisa wa JWTZ wakiendelea na shughuli za kuaga mwili wa marehemu kabla ya mazishi.
Heshima zikiendelea kutolewa.
Mjane wa marehemu akitoa heshima za mwisho kwa mume wake.

Jeneza lenye mwili wa marehemu likishushwa kaburini.
No comments