MBUNGE MWAKIBETE ACHANGIA MILIONI 10 UJENZI WA OFISI YA CCM BUSOKELO MBEYA
Mbunge wa Jimbo la Busokelo Atupele Mwakibete
..........................................
Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Jimbo la Busokelo Atupele Mwakibete amechangia kiasi cha Sh.Milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Busokelo.
Mwakibete amesema ameunga mkono jitihada hizo za kuchangia ujenzi wa ofisi hiyo kwa lengo la kuchochea maendeleo ya chama hicho na kuwaomba wanachama na wakereketwa kuchangia fedha ili kukamilisha ujenzi huo.
" Niwaombe wanachama wenzangu na wadau wengine kujitokeza kuchangia ujenzi wa ofisi hii ya chama chetu CCM," alisema Mwakibete.
No comments