JIJI LA DAR ES SALAAM KUFUNGWA TAA ZA BARABARANI 213
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabellya wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba huo iliyofanyika Disemba 28, 2024.
.............................................
Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
JIJI la Dar es Salaam linarajia kufungwa taa 213 za barabarani kufuatia kusainiwa kwa mkataba wa makubaliano wa ufungaji wa taa hizo.
Hafla ya utiaji wa saini wa mkataba huo imefanyika Disemba 28, 2024 baina ya jiji la Dar es Salaam na Kampuni ya M/S EH Enginerring Company Ltd ambayo itafunga taa hizo ambapo Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabellya ameshiriki katika utiaji saini wa mkataba huo.
Hafla hiyo ilikwenda sanjari na zoezi la uzinduzi wa uwashaji wa taa za barabarani katika eneo la soko la Machinga.
Akizungumza baada ya utiaji saini wa mkataba huo Mkurugenzi Mabelya alisema zitafungwa taa na kamera katika barabarani za jiji letu katika utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alilolitoa wakati wa ziara yake ya hivi karibuni mkoani Dar es salaam.
" Halmashauri ya Jiji tuna uhitaji wa taa 37,847 kwenye mitaa 159 yenye barabara zenye urefu wa kilomita 1,135.405 na mpaka sasa tayari taa 2,238 na kati ya taa hizo taa zinazotumia sola ni 1,926 na taa za umeme ni 312," alisema Mabelya.
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabellya akizungumza baada ya kushiriki katika utiaji saini wa mkataba huo.Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabellya akimkabidhi mkataba huo wakilishi wa Kampuni ya M/S EH Enginerring Company Ltd ambayo itafunga taa hizo.

No comments