Breaking News

MBETO: WANAMICHEZO ZANZIBAR WAKATI NI HUU

Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC   Zaanzibar ,Idara  ya Itikadi  ,Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto  Khamis  akisalimiana na wachezaji kabla ya kuanza mechi ya fainali ya kombe la Abdulghafar  jimbo la Mtoni  Mkoa Mjini Magharibi.

........................................ 

Na Mwandishi  Maalum , Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi  (CCM ) kimewataka wanamichezo Zanzibar , kuchangamkia fursa  zilizopo katika utawala wa SMZ   awamu ya nane kuweka  bidii na kuonyesha vipaji  vyao ili kuwa kucheza ngazi za kimataifa.

Ushauri  huo  umetolewa na Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC   Zaanzibar ,Idara  ya Itikadi  ,Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto  Khamis  wakati  kabla ya kuanza mechi ya fainali ya kombe la Abdulghafar  jimbo la Mtoni  Mkoa Mjini Magharibi.

Jimbo la Mtoni linaoongozwa na Mbunge  wake Abdulghafar Idrisa

Mbeto  alisema  wanamichezo wote katika   uongozi wa Rais wa Zanzibar  Dk Hussein  Ali  Mwinyi, wamepata bahati ya kujengwa  viwanja vya kisasa vya soka huku Rais akiwa  ndiye  mdau Mkuu wa  Michezo.

Alisema  kila akitazama kwa wakati huu  ,anatamani ingerudi   enzi  ya kushamiri kwa  viwango soka  zanzibar kwa timu  kama  Mwembelendu, Miembeni  Vikokotoni, Ujamaa, Navy  na Kikwajuni.

Timu nyingine zilizokuja kuwika baadae  Malindi, Black Fighters, Jamhuri, Small Simba, Shangani na  Mlandege huku akisema Zanzibar  ingepata soko la kuuza  wachezaji  wake   wengi duniani.

Mbeto alisema hata hivyo  zanzibar bado ina  nafasi kubwa kwa  wachezaji wake kujutuma na kutumia nafasi zilizopo  kujijenga kiuchumi kupitia   soka, kuogelea, riadha ,masumbwi na michezo  mingine kadhaa.

"Serikali imefanya kila linalowezekana na Zanzibar  inatambuliwa na caf .Itatacheza michuano ya cecafa kama Zanzibar . Ukitambuliwa Cecafa  umetambuliwa  Fifa. Wales, Scotland,  Northern Island na England  zinacheza kombe la dunia zikiwa nchi za Muungano UK, " alisema Mbeto.

Aidha  Katibu huyo Mwenezi,  alisema CCM kitaendelea kusimamia  sera  zake katika  kuinua  michezo  ili kuwafanya  wanamichezo waishi maisha bora kupitia jasho na  vipaji  vyao.

Hata hivyo  alisema  chama kimeielwlza SMZ  kupitoa waziri wake  dhamana ya  michezo   , kupeleka  wanamuziki wa taarab asilia kwenye  nchi za Misri na UAE  ili kuongeza mbinu na  ujuzi wa  muziki huo .

"Huwezi kuitenganisha Zanzibar na muziki  wa taarab .Maisha ya watu  wake na  mioyo yao huburudika kwa muziki wa taarab ulioipa sifa  Zanzibar kona zote duniani "alisema Mbeto.

No comments