Breaking News

MBETO : JUSSA FUTA NDOTO ACT WAZALENDO KUINGIA IKULU

Katibu  wa Kamati Maalum ya  NEC Zanzibar ,Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo , Khamis  Mbeto  Khamis, akizungumza wakati akijibu madai  yaliotolewa na Jussa  katika  mkutano  wa hadhara uliofanyika Kibandamaiti  Kisiwani Unguja. 

........................................ 

Na Mwandishi  Maalum , Zanzibar 

CHAMA Cha Mpinduzi (CCM) kimesema kwa vyovyote   ACT  Wazalendo  hakina wezo wa kuishinda   CCM na kumuondoa Rais aliye madarakani Zanzibar  Dk Hussein Ali Mwinyi.

Pia kimemkanya Makamu Mwenyekiti  wa ACT  Wazalendo, Ismail Jussa Ladhu, kutoidanganya  dunia, kuwapa matuimaini hewa wafuasi  wao kwa kufikiria  mambo yasiowezekana.

Onyo hilo limetolewa na Katibu  wa Kamati Maalum ya  NEC Zanzibar ,Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo , Khamis  Mbeto  Khamis , alipokijibu madai  yaliotolewa na Jussa  katika  mkutano  wa hadhara uliofanyika Kibandamaiti  Kisiwani Unguja. 

Mbeto alisema CCM hakijawahi kuwa na nakisi ya kura zake za  ushindi mwaka 2025  ,pia  si wana  CCM   Zanzibar au Tanzania , wanaoupinga utawala aidha  wa  Rais Dk  Samia Suluhu  Hassan au Rais Dk. Mwinyi .

Alimtaja  Jussa ndiye asiyekubalika ndani ya ACT kutokana na aina ya uongozi wake uliokigawa chama hicho  kati ya viongozi waasisi na wapya .

"Jusa amejitumia ujumbe unaohusu  aina  ya uongozi na siasa zisizokubalika ndani ya   ACT. Aache kujenga himaya mpya ma kuwagawa watu.  Asitake sauti  yake iwe uamuzi kuliko  vikao na katiba  ya ACT "alisema Mbeto.

Alisema CCM  kina taarifa za kutosha  za  kiongozi  huyo asivyokubalika , alivyojipanga  kuunda ACT a ndani ya ACT  huku akiishi  kwa kupigiwa debe na  mjane wa Hayati Maalim  Seif  Mama Awena Sinani .

"Jussa  hatakiwi  ndani ya ACT .Anaishi kwa  ushawishi na  heshima  ya Mama Awena. Wenzake  hawamtaki kwa jeuri , kibri na kujifanya kwake kujua kila kitu .Jussa hawezi kuwachagulia Rais  wazanzibari  wasiyemtaka" alisema.

Aidha  Katibu  huyo Mwenezi  CCM Zanzibar, alisema Jussa   asidhani kama atamudu kuvivaa viatu  vilivyoachwa na   Maalim seif  sharif Hamad vikamtosha kwa ujuvi  alionao , kutoambilika huku akikwepa kuoa.

'Mfikishieni salamu jussa  aache kujifanya anajua wakati   yeye mwenyewe hajijui .  Wenzake wamemsusa wakitaka abaki na kundi la wahamiaji  . Kumtenga  Juma Duni Haji na waasisi wengine kumewakera wengi  Act " alieleza.

Mbeto alisema  wakati wa kuihadaa dunia kama zamani , wananchi wakiishi  kwa hofu na wasiwasi umepita .Wati  wameshuhudia kazi kubwa inayofanywa na Rais Dk Mwinyi  toka ashike madaraka  

No comments