MSD TANGA YAPONGEZWA KWA MABORESHO YA USAMBAZAJI BIDHAA ZA AFYA KWA WAKATI
Meneja Huduma za Sheria wa Bohari ya Dawa (MSD), Elisamehe Macha (katikati) akizungumza na Watumishi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo, ambao ni wateja wa MSD wakati wa ziara iliyofanyika Septemba 3, 2024. Kutoka kushoto ni Meneja wa MSD Kanda ya Tanga, Sitti Abdurhaman na kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD ambaye pia ni Mlezi wa MSD kanda hiyo, Dkt. Rukia Mwifunyi.
.....................................
Na Dotto Mwaibale,
Tanga
WATEJA wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Tanga wameipongeza MSD kwa maboresho makubwa inayoendelea kuyafanya ya usambazaji wa bidhaa za afya kwa wakati.
Pongezi hizo wamezitoa kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD ambaye pia ni Mlezi wa MSD kanda hiyo, Dkt. Rukia Mwifunyi anayoifanya mkoani humo, kuzungumza na wateja wanaowahudumia ili kupata maoni yao juu ya huduma za MSD na kupokea changamoto zao ili ziweze kufanyiwa kazi.
Ziara hiyo inafanyika ikiwa ni moja ya matukio ya kuadhimisha miaka 30 ya utendaji wa MSD tangu 1994,ambapo kabla ya hapo ilikuwa ikiitwa Central Medical Store (CMS)
Mfamasia wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga (Bombo), Kibwana Mgude alipongeza MSD kwa kuwafikishia bidhaa za afya kwa wakati na kueleza kuwa sasa upatikanaji wa bidhaa za afya umeboreshwa kwa kiwango cha juu.
“ Sasa hivi tunapokea dawa na vifaa tiba kwa wakati tunakila sababu ya kupongeza maboresho haya ya MSD,” alisema Mgude.
Kwa upande wake Magdalena Chambo ambaye ni Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Nkumba alisema utaratibu unaofanywa na MSD wa kuwapelekea bidhaa za afya hadi vituoni mara sita (6) kwa mwaka ni mzuri.
Dkt. Mwifunyi akizungumza wakati wa ziara hiyo alipongeza MSD kwa kazi kubwa wanayoifanya ambapo alitumia nafasi hiyo kuomba kudumisha ushirikiano baina yao na wateja wao wanaowahudumia.Aliwasisitiza wateja hao wa MSD kutoa mapendekezo yao ambayo wataona yana tija kwa ajili ya kuboresha shughuli zinazofanywa na MSD.
“ Utoaji wa huduma bora za usambaji wa vifaa tiba na dawa ni jambo jema kwani jamii na taifa wanatutegemea,” alisema Dkt. Mwifunyi.
Katika ziara hiyo Dkt.
Mwifunyi aliongozana na baadhi ya maafisa wa MSD kutoka Kanda ya Tanga na Makao
Makuu wakiongozwa na Meneja Huduma za Sheria MSD, Elisamehe Macha,
MenejaMawasiliano naUhusiano wa MSD Bi. Etty Kusiluka na Meneja Huduma kwa Wateja
Dkt. Pamella Sawa.
Kikao cha MSD na wateja wao Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kikiendelea
Picha ya pamoja baada ya kikao hicho.
Safari ya kutembelea baadhi ya maeneo ya Hospitali ikifanyika.
Mfamasia wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga (Bombo), Kibwana Mgude (kushoto) akitoa maelezo ya jinsi ya uhifadhi wa bidhaa za afya katika Hospitali hiyo.
Picha ya pamoja baada ya kufanya mazungumzo na Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Nkumba, Magdalena Chambo.
Mguu na njia wakati wa kwenda kutembelea baadhi ya idara za Hospitali ya Mkoa wa Tanga (Bombo) wakati wa ziara hiyo.
No comments