Breaking News

KANISA LAMPA TUZO MBUNGE JIMBO LA BUSOKELO KUTAMBUA MAENDELEO YALIYOFANYIKA

Mbunge wa Jimbo la Busokelo Mheshimiwa Atupele Fredy Mwakibete

...............................................

Na Mwandishi Wetu, Rungwe
 

Katika Ibada ya Mwaka Mpya Iliyofanyika Katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God JCC Lwangwa imetambua kazi zinazofanywa na Mbunge wa Jimbo la Busokelo Atupele Fredy Mwakibete na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Ibada hiyo iliyoongozwa na Mchungaji Kelvin Kwileka imefanya maombi maalum kwa viongozi akiwemo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Dkt. Phillip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Busokelo Atupele Fredy Mwakibete, kisha kukabidhi tuzo kama ishara ya kutambua kazi iliyotukuka na inayoonekana jimboni inayofanywa na viongozi hao.

Aidha, Katika Ibada Hiyo Mheshimiwa Mwakibete amelishukuru Kanisa kwa maombi hayo pamoja na tuzo ya kutambua kazi inayofanywa na serikali ya awamu ya sita,pia ameweza kuchangia ujenzi wa ofisi ya mchungaji unaondelea kwa pesa Taslimu Shilingi Milioni Moja na Tripu Tano za Mchanga.

No comments