RAIS MWINYI: SERIKALI ITAENDELEA KUJENGA NYUMBA ZA KISASA ZA WANANCHI
.................................................
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali
Mwinyi amewathibitishia Wananchi kuwa Serikali itaendelea Kujenga Nyumba za
Kisasa Maeneo yote ambayo yana Nyumba
zilizo Chakavu kwa lengo la kuwapatia Wananchi Makaazi bora.
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo katika Ufunguzi wa Nyumba 72 za Makaazi na
Biashara Mombasa kwa Mchina
Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi zilizojengwa na Shirika la
Nyumba la Zanzibar.
Rais Dk.Mwinyi ameiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi kuandaa Mpango Maalum wa Kisheria wa Matunzo ya Nyumba inazozijenga ili Suala la Matunzo kuwa la
Lazima na Sio hiyari.
Rais Dk. Mwinyi amefahamisha
kuwa Mpango huo ni lazima Uzingatie
Mifumo ya Maji, Masuala ya Usafi na Uangalizi wa Nyumba zenyewe Ili ziendelee
kuwa na Haiba nzuri ilizonazo hivi sasa.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi amewashauri
Wamiliki wa Nyumba hizo kuanzisha Kamati Maalum za Matunzo ya Nyumba hizo kwa kila Mmiliki kuwajibika na Usafi na
Matunzo ya Nyumba anayomiliki.
Rais Dk.Mwinyi amesisitiza kuwa Wananchi ni lazima Wakubali kupisha Miradi ya Ujenzi wa Nyumba na kwamba Serikali itawafidia Nyumba Bora za Makaazi badala ya Fedha .
Halikadhalika Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuwa
Wananchi Kukaa katika Makaazi mazuri ndio dhamira ya Serikali na kuwa Mpango wa Ujenzi wa Nyumba 3000 eneo
la Chumbuni utaendelea katika
maeneo mengine na kuwaambia Wakaazi wa Kikwajuni kukaa
tayari kwani nyumba mia tano zitajengwa
katika eneo hilo na Serikali ipo
tayari kwa Mradi huo.
Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuridhika na Utendaji wa Wizara hiyo kwa Mafanikio Makubwa ya Miradi ya Ujenzi wa
Nyumba.






.jpg)




No comments