Breaking News

RAIS MWINYI: KILA MWANANCHI KULIPWA FIDIA ANAYOSTAHILI


.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewahakikishia Wananchi kuwa Serikali itamlipa kila Mwananchi  haki yake na hakuna  Mwananchi atakae sononeka kwa Kukosa fidia.

Rais Dk. Mwinyi ametoa agizo la Kila Mwananchi Kulipwa kile anachotaka ikiwa Malipo ya Fedha au Nyumba.

"Kila Mwananchi atalipwa kwa kile anachotaka wa fedha alipwe fedha na  anaetaka nyumba atalipwa nyumba" amesisitiza Dk. Mwinyi.

 Rais Dkt. Mwinyi  ameyasema hayo alipoweka Jiwe la Msingi Mradi wa Nyumba 370 za  Maakazi ziliopo Mangapwani Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa ni Nyumba za fidia kwa Wananchi walioathirika na Ujenzi wa Barabara katika Eneo la Mangapwani ikiwa ni sehemu  ya Ujenzi wa Bandari Jumuishi ya Mangapwani.

Rais Dkt. Mwinyi amewahimiza Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Kuchangamkia  Fursa za Kiuchumi zitakazokuwepo kwenye Miradi  mikubwa ya Maendeleo iliyomo Mkoani humo.

Akizungungumzia Ujenzi wa Bandari ya Mangapwani ameeleza kuwa tayari Mkandarasi  amelipwa malipo ya awali  na ameanza kazi za upimaji wa sampuli za  udongo katika eneo hilo  kuelekea kuanza ujenzi.

Vilevile, Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inakusudia kujenga  Uwanja Mkubwa wa Michezo (Football Academy) katika Mkoa wa Kaskazini Unguja utakaokuwa na Viwango vya Kisasa.

Rais Dkt. Mwinyi ametoa pongezi kwa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wakala wa Majengo ZBA  kwa Usimamizi mzuri uliofanikisha Ujenzi wa Nyumba hizo pamoja na  Mkandarasi wa Ujenzi huo Kampuni ya ORKUN ya Uturuki.

No comments