RAIS MWINYI: JENGO JIPYA LA ZEC KUIMARISHA DEMOKRASIA ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali
Mwinyi amesema Ujenzi wa Jengo jipya la Tume ya Uchaguzi unalenga Kuiimarisha Mifumo ya Kidemokrasia Nchini .
Rais Dk, Mwinyi ameyasema hayo alipoweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo
la Afisi Kuu ya Tume ya Uchaguzi Maisara
,Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Aidha Rais Mwinyi ameeleza kuwa Kukamilika kwa Jengo hilo kutamaliźa
tatizo Sugu la Muda mrefu lililoikabili Tume ya Uchaguzi (ZEC) la
kutokuwa na eneo Bora la kufanyia kazi
zake.
Rais Dk.Mwinyi amefahamisha kuwa Uamuzi wa
kulifanya Jengo hilo kuwa Kituo kimoja cha Shughuli zote za Uchaguzi (
One Stop Centre) kutaongeza Ufanisi kwa Watendaji wa tume.
Halikadhalika , Rais Dk.Mwinyi ameipongeza Tume ya Uchaguzi na Wakala wa
Majengo (ZBA) kwa kazi nzuri ya Kusimamia Ujenzi huo kwa Viwango bora na kuihimiza Kampuni ya
CRJE ambao ndio Wakandarasi wa Ujenzi
huo kumaliza kazi kwa Wakati.
Naye, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa
ZEC Thabit Idarous Faina ameeleza kuwa
Ujenzi huo utakamilika na kuanza kutumika kabla ya Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba
Mwaka huu.
Ujenzi wa Majengo Mawili yenye Ghorofa nne
Utagharimu kiasi cha Takriban Shilingi Bilioni 11.32 utakapokamilika
Fedha zilizotolewa na Mfuko Mkuu wa Serikali, kwa sasa Ujenzi umekamilika kwa
Asilimia 81 .
Amefafanua kuwa Majengo hayo Mawili moja litatumika kwa Shughuli za Afisi
za Tume na jengine kwa ajili ya Huduma za Shughuli za Uchaguzi.Rais Dk, Mwinyi akivuta pazia kuashiria uwekaji jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Afisi Kuu ya Tume ya Uchaguzi Maisara ,Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
No comments