RAIS MWINYI:TAASISI YA SAYANSI ZA BAHARI UDSM INA MCHANGO MKUBWA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Taasisi ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ina Mchango Mkubwa katika Mipango na Sera za kuendeleza Uchumi wa Buluu unaozingatia matumizi endelevu ya rasilimali za Bahari.
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipoweka jiwe la Msingi Jengo la Taaluma na
Utawala la taasisi hiyo Buyu ,Wilaya ya Magharibi B ,Mkoa wa Mjini Magahribi.
Aidha Rais Mwinyi ameahidi Serikali kuendelea Kushirikiana na Taasisi hiyo
wakati wote kwa lengo la kuhakikisha
Rasilimali za Bahari ziliyopo zinatumika ipasavyo ili kutoa Mchango
Mkubwa kwa Uchumi na Ustawi wa jamii.
Amefahamisha kuwa kuimarika kwa
Miundombinu ya Taasisi hiyo hapa Zanzibar kutatoa mchango mkubwa wa sekta nyengine
muhimu ziliyomo katika Uchumi wa Buluu.
Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa matarajio ya Serikali ni kuona Sekta ya Utalii inayochangia asilimia
30 ya Uchumi wa nchi ,Uvuvi ,Ukulima wa Mwani
na Mazao ya Baharini zinaimarika
kupitia Tafiti zitakazoandaliwa na Taasisi hiyo pamoja kutoa Wataalamu
wenye weledi watakaojifunza katika taasis hiyo.
Amezitaja sekta nyengine kuwa ni
Bandari, Mafuta na Gesi na Usafiri wa
Baharini.
Ameyalezea Matarajio mengine kuwa ni kwa Taasisi hiyo Kufanya Tafiti za Uchumi wa Buluu zitakazotoa
Matokeo bora kwa ajili ya Uandaaji wa Sera na Mipango ya Maendeleo ya
Sekta hiyo.
Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ametumia fursa hiyo kuishukuru Benki ya Dunia
kwa Mchango wao katika miradi mingi ya
Maendeleo nchini kitendo kinachoonesha
Kuaminika kwa Serikali zote mbili za SMT na SMZ kutokana na Matumizi mazuri ya
fedha za Miradi ya MaenÄeleo na Kuwasisitiza kuendelea na Mchango huo.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi ametoa rai kwa Wawekezaji kulitumia Eneo la Buyu kuchangamkia Fursa
za Uwekezaji kutokana na Mandhari nzuri ya eneo hilo
kwa Makaazi na Malazi kwa Wanafunzi ,Huduma za Usafiri ,Kumbi za
Mikutano ,Huduma za Utafiti ,Hospitali , Utafiti wa Bahari na Shughuli mbalimbali za Kijamii.
No comments