DC KILINDI AWASHAURI MADIWANI KUHAMASISHA WAZAZI KUITANGAZA MIRADI ILIYOTEKELEZWA
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Hashim Mgandilwa akizungumza.
.............................................
Mashaka Kibaya,Tanga.
MADIWANI wa halmashauri ya Kilindi wametakiwa kuhamasisha wazazi kuwapeleka watoto wao shule ili kuweza kuleta tija kwenye uwekezaji mkubwa uliofanywa kwenye sekta ya elimu na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Katika mkutano wa baraza la Madiwani uliyofanyika jana, Mkuu wa wilaya ya Kilindi Hashim Mgandilwa alitoa rai hiyo alipopatiwa fursa ya kuweza kuwasilisha salaam za Serikali kwa Wajumbe.
Alisema, kumekuwa na nwamko mdogo kwa Wazazi kuwapeleka watoto wao shule licha ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya elimu.
Kutokana na hali hiyo amewaimba madiwani kufanya kazi ya kuhamasisha wazazi kuwapeleka watoto wao shule hatua ambayo itasaidia katika kuleta tija kwenye miradi hiyo waliyopatiwa na Serikali.
"Rais ametoa mchango mkubwa sekta ya elimu, hivi sasa tunazo shule nyingi hata zenye kidato cha tano na Sita,kuna Mkindi, Kikunde na nyingine lakini bado unapnekana kuna changamoto wazazi kuwapeleka watoto shule"alisema Mgandilwa.
Alisema kuwa, madiwani watakapo hamasisha wazazi kuwapeleka watoto shule,uwekezaji uliofanywa na Serikali kwenye sekta ya elimu utaleta matokeo chanya, akiongeza kusema kuwa elimu ni muhimu katika kipindi kilichopo.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya ya Kilindi alizungumzia suala la umuhimu wa ukusanyaji mapato, akiwataka madiwani kuhakikisha halmashauri yao inakusanya kwa kiasi cha asilimia mia moja.
Vile vile Mkuu huyo wa wilaya ya Kilindi aliwataka Wajumbe wa baraza la madiwani kwenda kuhamasisha Wananchi ili waweze kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu ili wapiga kura ili waweze kupata fursa ya kuchagua viongozi wao kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Mgandilwa pia aliwasihi madiwani kwenda kuendelea kutekeleza wajibu wao wa kuwahudumia Wananchi hususani kwenye suala zima la usimamizi wa miradi ya mbalimbali maendeleo kwenye maeneo yao.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kilindi, Rajabu Kumbi, aliwataka madiwani kwenda kufanya kazi pasipo ya kulalamika akiwasisitiza kuhakikisha ushauru unakusanya huku wakibuni vyanzo vipya vya ukusanyaji mapato.
No comments