Breaking News

HALMASHAURI YA WILAYA YA KILINDI YAJIDHATITI UKUSANYAJI WA MAPATO

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani hivi karibuni.

...................................................

Na Mashaka Kibaya,Kilindi 


HALMASHAURI ya Wilaya ya Kilindi Mkoa wa Tanga imenunua mashine za Posi mia moja (100) ikiwa ni sehemu ya kujidhatiti katika suala la ukusanyaji wa mapato ya ndani, Mkuruhenzi mtendaji John Mgalula ameeleza.

Katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika jana wilayani humo, Mgalula alisema kwamba, halmashauri imenunua mashine hizo kusaidia ukusanyaji ushauru na pia zikisaidia kuziba mianya ya upotevu mapato ya Serikali.

Mgalula alisema mashine hizo zilizonunuliwa na zile zilizokiwepo hapo awali zinatimiza idadi  Posi 146 huku Saba (7) jitihada ambazo zinaaminika katika ukusanyaji wa mapato.

Kwa mujibu wa Mgalula mashine hizo zitatolewa kwa wazabuni, watendaji kata na vijiji ili kutekeleza majukumu ya kukusanya mapato kwenye vizuizi vya mazao (mageti) na minada.

Awali akiwasilisha salaam za Serikali kwenye baraza la madiwani, Mkuu wa wilaya ya Kilindi Hashim Mgandilwa aliwapongeza wajumbe kwa kazi kubwa ya usimamizi utekelezaji miradi ya maendeleo.

Aidha alisema kuwa, katika mwaka 2024 halmashauri ya Kilindi ilikusanya mapato kwa asilimia 131% hatua ambayo ilitoa fursa ya utekelezwaji wa miradi ya ziada kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

"Mwaka 2024 tulikuaanya asilimia 131% na kutoa fursa ya kutekeleza miradi mingi hata isiyokuwepo kwenye mipango yetu, tujikite kwenye ukusanyaji mapato kwa asilimia 100% ili kufikia malengo" alisema Mkuu huyo wa wilaya.

Akitilia msisitizo suala la ukusanyaji mapato Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilindi, Idrisa Mgaza alisema, kukosekana kwa mapato ni matokeo ya halmashauri kutokuwepo.

Mgaza amewataka wale wote wenye dhamana ya kukusanya mapato, kwenda kuwajibika kikamilifu hatua ambayo pia itawasaidia kukusanya kwa wingi na halmashauri kunufaika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilayani Kilindi, Rajabu Kumbi, aliwataka madiwani kuendelea kufanya kazi kwa bidii huku akiwasihi kuwaelimisha wananchi juu ya kujiandaa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa wanapoendesha kilimo.

Kumbi alisema kwamba,hali ya hewa inabadilika mara kwa mara, hivyo Madiwani wanapaswa kuwashauri wananchi kutumia mbegu bora zikiwemo zile zinazohimiki ukame sambamba na kuwatumia wataalam wa kilimo.

Kikao hicho kikiendelea.

Taswira ya kikao hicho.
 

No comments