POLISI MKOA WA SONGWE WAMKAMATA RAIA WA MALAWI AKIWA NA MENO YA TEMBO
.........................................
Na Mwandishi Wetu, Songwe
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Songwe limemkamata mwanaume mmoja kwa tuhuma za kupatikana na
nyara za serikali meno ya tembo.
Ni kwamba Februari 16, 2025 saa 04:30 usiku huko
Kitongoji cha Msia, Kata ya Chitete, Tarafa ya Bulambya Wilaya ya Ileje, Mkoa
wa Songwe, Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kupitia taarifa za kiintelijensia
pamoja na misako na doria za mara kwa mara zinazoendelea kufanyika ikiwa ni
pamoja na kushirikiana na Idara mbalimbali ikwemo Mamlaka ya Usimamizi wa
Wanyamapori Tanzania - TAWA Wilaya ya Ileje.
Jeshi hilo limefanikiwa kumkamata
Chisamba Siame Kameme (60) Mkukima, raia wa nchi ya Malawi akiwa na vipande 18
vya meno ya tembo yenye thamani ya 84.2Kg na baada ya kufanya tathimini na
wataalam ilionesha kuwa thamani ya meno hayo ni kiasi cha Shilingi Milioni
153,540,000 (Milioni Miamoja Hamsini na Tatu Laki Tano na Arobaini Elfu) ikiwa
ni sawa na Tembo wa 03 na kila tembo 01 akiwa na thamani ya 51,180,000 (Milioni
Hamsini na Moja Laki Moja na Themanini Elfu) alivyokuwa ameviweka kwenye mfuko
wa sandurusi alizozipakia kwenye baiskeli akittafuta wateja wa kuwauzia..
Aidha, Shauri la kesi hii upelelezi bado
unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
Jesh la Polisi Mkoa wa
Songwe, linatoa wito kwa baadhi ya mtu au watu wenye tabia ya kufanya uhalifu
wa kijangili kwa wanyama pori ambao ni kinyume na sheria kuacha mara moja kwani
halitosita kuwachukulia hatua wale wote wenye tabia kama hiyo ikiwa ni pamoja
na kuwafikisha mahakamani ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama
hizo. imeelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishina Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga.
No comments