TANESCO SINGIDA YAFANYA BONANZA KUAGA MWAKA 2024, WAAHIDI UFANISI WA KAZI 2025
Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Singida, Mhandisi Boniface Shitindi akizungumza wakati wa Bonanza la Wafanyakazi wa shirika hilo lililofanyika Februari 15, 2025.
........................................
Na Dotto
Mwaibale, Singida
WAFANYAKAZI
wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Singida wamefanya bonanza la
michezo mbalimbali kwa ajili ya kuuaga mwaka 2024 na kukaribisha mwaka 2025.
Kaimu Meneja
wa Tanesco Mkoa wa Singida, Mhandisi Boniface Shitindi amesema lengo la kufanya
bonaza hilo ni kuimarisha afya zao ili waweze kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni
juhudi za kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia
Suluhu Hassan.
“
Tunapofanya kazi kwa bidii tunakuwa tunainua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa
kwa ujumla kwa hiyo bonanza hili ni chachu kwa wafanyakazi wa Tanesco chini ya
Mkurugenzi wetu Mkuu Mhandisi Gissima Nyamohanga ambaye wakati wote amekuwa akisisitiza umuhimu wa
kufanya kazi kwa kujituma,” alisema Shitindi.
Shitindi
alisema kufanyika kwa bonanza hilo ni utaratibu wa shirika hilo kila mwaka kwa
nchi nzima na limekuwa na manufaa makubwa kwa kuwa limekuwa likiwakumbusha
wafanyakazi kutekeleza majukumu yao ya kazi vizuri.
Alitaja
baadhi ya michezo iliyofanyika katika bonanza hilo kuwa ni mpira wa miguu,
kutembea kwenye vibao, kukimbiza kuku
kwa wanaume na wanawake, kurusha mkuki, kuzunguka viti na kukaa, kufungwa
kitambaa usoni,kutafuta vitu,riadha kwa kukimbia mita 100, 300 hadi 600 na mchezo wa drafti.
Wakizungumza
kwa niaba ya wenzao washiriki wa bonanza hilo, Siah Mmari, Recardo Fifi na
Ibrahim Solo walipongeza uongozi wa shirika hilo kwa kuanzisha bonanza hilo
ambalo limekuwa likiwajenga kiafya na kuwafanya kuwa na mori wa kufanya kazi
kwa bidii.
“Bonanza
hili limekuwa likitujenga kiafya na kubadilisha mawazo kwa wafanyakazi kwa
kujumuika pamoja kutoka wilaya zote na limekuwa likiwafanya kuwa na mori wa
kufanya kazi,” alisema Ibrahim Solo.
Shamim Mohamed kutoka Manispaa alisema kwa mwaka huu wa 2025 wamaahidi kufanya kazi kwa ufanisi zaidi ikiwa ni utekelezaji wa Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan ambaye anahimiza utendaji kazi.
Washindi wa
michezo mbalimbali katika bonanza hilo ni Recardo Fifi kutoka Wilaya ya Itigi
ambaye alijinyakulia kitoweo cha kuku baada ya kushinda mchezo wa kukimbiza
kuku kwa upande wa wanaume ambapo kwa upande wa wanawake alikuwa ni Hidaya Rashid.
Katika
mchezo wa kurusha mkuki alikuwa ni Yohana Wambura kutoka Kiomboi Wilaya ya
Iramba wakati mshindi wa kuzunguka viti na kukaa kwa upande wa Wanaume akiwa ni Yohana
Wambura na mshindi kwa wanawake akiwa ni
Shamim Mohamed kutoka Manispaa ya Singida.
Washindi
wengine ni wa kutafuta vitu huku wakiwa wamefungwa kitambaa usoni ambapo kwa
upande wa wanaume alikuwa ni Bakari Said kutoka Wilaya ya Ikungi na kwa
wanawake akiwa ni Siah Mmari kutoka Manispaa ya Singida.
Kwa upande wa riadha mshindi alikuwa ni Issa Iddi ambaye alishinda kwa kukimbia umbali wa mita 100 na mshindi wa pili kwa upande wa wanaume akiwa ni Edward Mizengo kutoka Wilaya ya Manyoni na mshindi kwa upande wa wanawake akiwa ni Siah Mmari ambaye alikimbia umbali wa mita 100, ambapo kwa umbali wa mita 300 akiwa ni Patricia Sausi,
Katika
mchezo wa kutembea kwenye vibao mshindi alikuwa ni Selemani Lutavi kutoka Kiomboi
huku Shamim Mohamed kutoka Manispaa akishinda mchezo wa kuzunguka viti na kukaa.
Kwa mpira wa
miguu timu ya Manispaa ya Singida ikiibuka mshindi kwa magori 2-1 dhidi ya timu
ya kutoka wilaya zote.
Katika mchezo wa drafti aliyeibuka mshindi ni Mhandisi, Ernest Nyerere.
Afisa Huduma kwa Wateja Tanesco Mkoa wa Singida, Ibrahim Solo akizungumza wakati wa bonanza hilo.
Wachezaji wa Timu ya Manispaa ya Singida wakiwa katika picha ya pamoja.
Wachezaji wa Timu ya Tanesco kutoka wilaya zote za Singida wakiwa katika picha ya pamoja.
Mchezo wa Drafti ukifanyika katika bonanza hilo.
Mchezo wa kutembea kwenye vibao ukifanyika. Kulia ni mshindi wa mchezo huo, Selemani Lutavi.
Ukimbizaji kuku ukifanyika. Katikati ni Dereva wa shirika hilo, Widony Chisoma alionesha umahiri wa kukimbiza kuku kwa ajili ya kitoweo.
Mchezo wa kuzunguka viti na kukaa ukifanyika.
Ukaaji kwenye kuku ukifanyika, Kutoka kushoto ni Ricardo Fifi na kulia ni Yohana Wambura kutoka Kiomboi Wilaya ya Iramba. |
Mshindi wa kukimbia mita 100 kwa upande wa wanawake, Siah Mmari akionesha umahiri wa kukimbia.
Mshindi wa kwanza wa kukimbia mita 600, Hamisi Mtangi akionesho uwezo wake wa kukimbia.
Picha za pamoja na Kaimu Meneja wa Tanesco Singida na viongozi wengine
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Kaimu Meneja wa Shirika hilo Mkoa wa Singida, Mhandisi Boniface Shitindi akikabidhiwa zawadi ya kitoweo cha kuku. Kulia ni Katibu wa Kamati ya Bonanza hilo, Yusra Nicholaus.
No comments