Breaking News

KAMPUNI ZA EMIRATES LEISURE NA DNATA ZATOA MSAADA KWA KITUO CHA WAHITAJI ZANZIBAR

Wafanya kazi wa Kampuni za  za Emirates Leisure na DNATA Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wenye uhitaji wa Kituo cha Markaz Lyaqiin Islamic Center kilichopo Kinduni Zanzibar baada ya kuwapatia msaada wa vitu mbalimbali.

.........................................

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar 

KAMPUNI za Emirates Leisure na DNATA Zanzibar zimetoa msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha Watoto Yatima cha Markaz Lyaqiin Islamic Center kilichopo Kinduni Zanzibar.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo, Meneja Mkazi wa Kampuni ya Emirates Leisure, Mr Paul Attallah alisema utoaji wa msaada huo ni mwendelezo wa kampuni hizo katika kuungamkono jitihada za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi za kuwajali wanananchi.

“ Msaada huu tunao utoa ni mwendelezo wa ratiba yetu ya  kuwashika mkono watu wenye uhitaji na pia kuunga mkono jitihada za Serikali ya Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye siku zote amekuwa akizitaka kampuni mbalimbali kuwa na utamaduni wa kurudisha kwa jamii faida wanayoipata kwa kuyasaidia makundi maalumu yenye uhitaji kwa lengo la kuwapa furaha, “ alisema Attallah.

Kwa upande wake Afisa Utawala wa Kampuni ya  Emirates Leisure, Msokolo Layya   alisisitiza kudumisha ushirikiano baina ya kampuni hizo na kueleza kuwa wataendelea kusimamia ratiba ya kutoa msaada kwa wahitaji katika kipindi cha mwaka mzima kama walivyopanga.

Katika hafla hiyo viongozi mbalimbali wa kampuni hizo walikuwepo wakiongozwa na Meneja Mkazi wa Kampuni ya  Emirates Leisure, Paul Attallah, Mkuu wa Fedha wa kampuni hiyo,  Noah Mwansa,  Shuwea,  Commacial Support wa DNATA, Kaimu Rasilimali Watu na Utawala wa Kampuni ya DNATA, Bi. Lucy na Afisa Utawala wa Emirates Leisure, Msokolo Layya.

Wengine wliohudhuri hafla hiyo ni wawakilishi toka kampuni hizo, Meneja Usafirishaji wa Kampuni ya DNATA, Anthony, Meneja wa Kampuni ya DNATA na Compliance Manager wa Kampuni ya DNATA, Mr George na Bi Zainab kutoka Kampuni ya DNATA.

Viongozi wa wa kituo hicho wamezishukuru kampuni hizo kwa msaada mkubwa walioutoa kwa ajili ya watoto hao wenye uhitaji.

Msaada huo ukikabidhiwa.
Msaada ukikabidhiwa kwa walengwaAfisa Utawala wa Kampuni ya  Emirates Leisure, Msokolo Layya  akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo.


No comments