KATIBU MKUU CHAMA CHA NLD ACHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Ibrahim Pogora akimkabidhi fomu Mgombea wa nafasi ya Urais wa chama hicho Doyo Hassan Doyo Makao Makuu ya chama hicho Tandika jijini Dar es Salaam Machi 20, 2025.
...................................................
Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
MGOMBEA nafasi ya Urais kupitia Chama cha NLD Mhe. Doyo Hassan Doyo leo Machi 20, 2025 amechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo na kueleza kwamba iwapo ataipata atafanya Mapinduzi makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo na kuinua uchumi nchini.
Amesema iwapo atapata nafasi hiyo kipaumbele chake kingine ni kumuendeleza mtoto wa kike katika elimu na teknolojia.
Aidha ametoa angalizo kwa watanzania kuepuka kauli za baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa ambazo zinaweza kuhatarisha amani ya nchi kuelekea uchaguzi mkuu utakofanyika mwezi oktoba mwaka huu na ameviomba vyombo vya dola visisite kuwachukulia hatua kali viongozi hao.
Doyo alitaja kauli mbiu ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu kuwa ni 'uzalendo haki na maendeleo'
Mhe. Doyo ameweka rekodi ya kuwa mtanzania wa kwanza kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025.
Mgombea nafasi ya Urais kupitia Chama cha NLD Mhe. Doyo Hassan Doyo, akionesha fomu baada ya kukabidhiwa. 
Mgombea nafasi ya Urais kupitia Chama cha NLD Mhe. Doyo Hassan Doyo, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa fomu. 

Mgombea nafasi ya Urais kupitia Chama cha NLD Mhe. Doyo Hassan Doyo akipunga mkono wakati akienda kuchukua fomu. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Taifa Tanzania Bara, Otheniel Mizizi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Ibrahim Pogora, akizungumza wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Mjumbe wa kamati ya uchaguzi, Sabra Massanza na kulia ni Katibu wa kamati ya uchaguzi, Doni Mnyamani.
Wanachama wa chama hicho wakiwa kwenye mkutano huo.
Hafla ya kukabidhiwa fomu hiyo ikiendelea.
Mkutano huo ukiendelea.










.jpg)




No comments