Breaking News

KATIBU MKUU NLD DOYO HASSAN DOYO KUCHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS

Katibu Mkuu wa Chama cha  National League for Democracy  (NLD) ambaye ni Mtia nia wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho Mhe. Doyo Hassan Doyo akizungumza katika moja ya mikutano yake na waandishi wa habari.

..............................................

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KATIBU Mkuu wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Mhe. Doyo Hassan Doyo ambaye ni Mtia nia wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho kesho anatarajia kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo

Hatua ya kuchukua fomu hiyo imekuja baada ya kutangaza rasmi nia yake ya kugombea nafasi hiyo ya uongozi wa juu wa nchi Machi 14,  2025, mjini Morogoro.

Kwa mujibu wa kanuni ya hicho, sura ya pili inamtaka mtangaza nia kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo ndani ya chama siku 14 kabla ya mkutano mkuu ili kutimiza matakwa ya chama kikanuni.

Kutokana na utaratibu huo Mhe. Doyo Hassan Doyo anatarajia kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo ndani ya chama kesho Machi 2025 kabla ya mkutano mkuu. 

Wanachama wa NLD na waandishi wa habari kwa pamoja wamekaribishwa kushiriki katika tukio hilo muhimu la kihistoria la uchukuaji fomu, litakalofanyika Machi 20, 2025, ofisi za chama hicho,Tandika Mtaa wa Lituhi, jijini Dar es Salaam, mkabala na Msikiti wa Watoto yatima, kuanzia Saa 4:00 asubuhi.

No comments