MBUNGE SUMA FYANDOMO ATOA SALAMU ZA SHUKURANI KWA WASIRA, AWATAKA WANA CCM MBEYA KUSHIKAMANA
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya, Suma Fyandomo akizungumza wakati akitoa Salamu za shukurani baada ya kumalizika kwa ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Ndugu Stephen Wasira aliyoifanya Mkoa wa Mbeya.
...........................................
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya. Suma Fyandomo ametoa
Salamu za shukurani baada ya kumalizika kwa ziara ya Makamu Mwenyekiti wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndugu Stephen Wasira aliyoifanya Mkoa wa
Mbeya hivi karibuni.
Aidha, Mbunge Fyandomo ameushukuru uongozi wa CCM Mkoa wa
Mbeya, wanachama wa CCM na wananchi kwa ushirikiano wao katika
kufanikisha ziara hiyo muhimu kwa chama na Taifa kwa kuzingatia kuwa chama
hicho ndicho kimeshika dola.
Fyandomo alitumia nafasi hiyo kupongeza hotuba ya makamu mwenyekiti huyo wa CCM Tanzania Bara aliyotoa wakati wa
ziara zake ndani ya Wilaya za Mkoa wa Mbeya na kueleza kuwa imeleta msukumo mpya wa maendeleo ya mkoani humo na kuwa maagizo aliyowapa watayatekeleza.
Hata hivyo, Fyandomo amewahimiza wana CCM mkoani Mbeya kuendelea
kushikamana na kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo ili kuimarisha maendeleo ya
jamii na kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi katika uchaguzi mkuu
utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Mbunge Fyandomo baada ya kutoa salamu hizo aliongoza zoezi
la ugawaji zawadi kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Ndugu Stephen
Wasira ambaye amehitimisha ziara yake mkoani humo na kuanza ziara ya kikazi
mkoani Kagera.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya, Suma Fyandomo akiongoza shamra shamra wakati wa ziara hiyo ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Stephen Wasira mkoani humo.

Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara Ndugu Stephen Wasira akipokea zawadi.









.jpg)




No comments