TANESCO YAPONGEZWA KUTEKELEZA AGIZO LA SERIKALI, YAZINDUA NAMBA MPYA YA HUDUMA KWA WATEJA -180
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga akihutubia wakati alipokuwa akizindua namba mpya ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ya kupiga simu bure kwa wateja ambayo ni 180 katika hafla iliyofanyika Machi 12, 2025 jijini Dar es Salaam.
.........................................
Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limepongezwa kwa
kutekeleza agizo la Serikali lilitolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko ambaye alilitaka shirika hio lihimarishe huduma ikiwemo la kupiga
simu bure bila ya malipo kwa ajili ya
maulizo na changamoto mbalimbali.
Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith
Kapinga wakati alipokuwa akizindua namba mpya ya kupiga simu bure kwa wateja
ambayo ni 180 alipokuwa akihutubia katika uzinduzi huo uliofanyika Machi 12,
2025 jijini Dar es Salaam.
Kapinga alisema lengo la namba hiyo ni kumuwezesha kila
mtanzania aweze kupiga simu wakati wote na kupata huduma kutoka Tanesco bila ya
kukatwa fedha na muda wake wa maongezi na kueleza kuwa hiyo ndio hadhima ya Serikali ya
kuwatumikia wananchi kwa viwango bora vya huduma.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Mhandisi Gissima Nyamo- Hanga akizungumza katika uzinduzi huo
alisema shirika hilo limefanya mageuzi makubwa katika utoaji wa huduma bora kwa
wateja kwa kuzindua namba hiyo ya simu
bila malipo kwa wateja na kuwa hayo ni mafanikio katika utoaji wa huduma kwa
wateja wao kwa makundi yote.
“ Shirika la Tanesco lina jumla ya wateja 5,330,023 hadi kufikia Januari 2025 nchi kote, wateja hawa
kwetu ni muhimu sana na ni sejemu ya mafanikio makubwa ndani ya shirika na
hivyo tumekua tukitafuta njia mbalimbali za kuhakikisha kuwa tunakua karibu na
kuwapa urahisi wa kupata huduma zetu ambapo wateja wanaweza kutufikia na
kuwasilisha changamoto zao,” alisema Mhandisi Nyamo-Hanga.
Alisema ukaribu huo na wateja ulianza kwa namba za kila mkoa
na kila wilaya kuwa na namba za dharura
ambazo zilikua zinapatikana masaa 24 na hivyo wateja kuweza kuwafikia muda
wote.
Kwa upande wake Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa
Tanesco, Balozi Zuhura Bundala alisema nishati ya umeme ndio kila kitu kwa
maisha ya mwanadamu na kueleza kuwa bila ya umeme tukianzia shughuli zetu
binafsi, na masuala ya biasha zote kuanzia za chini, za kati
na kubwa hazitaweza kufanyika.
Alisema kwa muktaza huo upatikanaji wa umeme ni muhimu na
usiwe tu wa kutosha bali uwe wa uhakika na pamoja na hayo yote huduma ya
upatikana wa umeme iwe nzuri kwa maana huduma bora kwa wateja ambapo alieza
uzinduzi wa namba hiyo mpya ya huduma kwa wateja imelenga kuboresha huduma ya
Tanesco kwa wateja wake.Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Mhandisi Gissima Nyamo- Hanga akizungumza katika uzinduzi huo.
Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco, Balozi Zuhura Bundala, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Mhandisi Gissima Nyamo- Hanga akiwa meza kuu na viongozi wengine.
Maafisa Huduma kwa Wateja wa Tanesco na wageni wengine mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Hafla ya uzinduzi huo ikiendelea
Uzinduzi ukiendelea
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Mhandisi Gissima Nyamo- Hanga, akimuelekeza jambo Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco, Balozi Zuhura Bundala.
Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco, Balozi Zuhura Bundala, akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya uzinduzi huo.
Wafanyakazi wa TANESCO wakifurahia kujipiga picha kuonesha furaha ya uzinduzi huo.
No comments