VETA KANDA YA DAR ES SALAAM YAJIVUNIA MAFANIKIO, FANI ZA WAVULANA ZA CHANGAMKIWA NA WASICHANA
Mratibu wa VETA Kanda ya Dar es Salaam, Florence .Kapinga akizungumza na waandishi wa habari Machi 13, 2025 kuhusu mafanikio ya VETA katika kipindi cha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake.
............................................
Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA) Kanda ya Dar es Salaam ikiwa katika maazimisho ya miaka 50 ya utoaji mafunzo na miaka 30 ya VETA Kanda hiyo ina jivunia mafanikio makubwa ya utoaji mafunzo ya ufundi katika fani mbalimbali.
Akizungumzia mafanikio ya VETA Kanda ya Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi wa kanda hiyo Wilhard Soko, Mratibu wa VETA Kanda ya Dar es Salaam, Florence .Kapinga alisema wanajivunia mafanikio makubwa walioyapata katika kipindi chote cha miaka 30 tangu kuanzishwa mwaka 1968 na kueleza mafanikio kadhaa waliyoyapata kwa kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa wameptana vifaa vipya vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),Vifaa vya Printing,Vifaa vya masomo ya Electronics na vitabu mbalimbali kwenye maktaba ya Chuo cha VETA Chang'ombe na Kipawa.
Amesema kumekua na ongezeko la udahili, ujenzi wa vyuo vipya vitatu na kufanya idadi yake kuwa vitano pamoja na vile vya awali ambavyo vinajengwa katika Wilaya ya Ubungo, Kinondoni na Kigamboni na kuwa ujenzi wake unaendelea na unatarajiwa kukamilika 2026.
Kapinga alitaja majukumu makubwa ya VETA Kanda ya Dar es Salaam ni kutoa mafunzo,kusimamia mafunzo,kuratibu mafunzo,kuhamasisha na kutahini wahitimu wa mafunzo kwa ngazi ya mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi ambapo kwa kwa mwaka wamefanikiwa kutahini wanafunzi wapatao 6,000 kwa kanda hiyo.
Alisema kuna ongezeko kubwa la wanafunzi wa kike kwa asilimia 30 ambao wanajiunga na fani za filter na umeme ambazo zamani zilikua zikionekana kuwa za wanaume.
Aidha, Kapinga ameeleza kuwa VETA Kanda ya Dar es Salaam wamekua na mashirikiano na wadau mbalimbali kama vile Benki ya KCB,VCO TZ, Airtel ,SKM Signal, pia wanafanya vipindi katika vyombo vya habari vikitangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Kanda ikiwemo kutangaza nafasi za masomo na kushiriki maonesho ya kazi mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi.
Ameeleza changomoto wanazokabiliana nazo kuwa ni uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi,fani mtambuka, kiingereza , mathematics, pamoja na vifaa vya kufundishia,uhaba wa majengo, nafasi finyu ya madarasa ukilinganisha na idadi ya wanafunzi.
Akizungumza kwenye maonesho ya vitendo yaliyoandaliwa katika Kanda ya Dar es Salaam Mwalimu wa Eletronic, Ricky Sambo amesema kwamba Kanda ya Dar es Salaam ina vituo vitatu vyakutolea mafunzo ambavyo ni Kanda ya Dar es Salaam ,Dar es Salaam na cha Kipawa ambacho ni mahusui kwa masomo ya TEHAMA.
Mafunzo yanayotolewa katika vyuo hivyo ni ya muda mfupi na ya muda mrefu katika fani za Umeme,Maabara,Ushonaji,Uchapaji,Uchoraji wa ramani na usanifu wa majengo, Electronics, ICT, Mechatronics,DSCT ,ufundi seremala, fani ya mabomba, uchomeleaji pamoja na ubunifu mbalimbali na maonesho hayo yaliaanza Machi 11 na yatahitimishwa Machi 14,2025 katika Viwanja vya VETA Chang'ombe Jijini Dar es Salaam.
Mwalimu Sambo amesema ada ya chuo kwa fani zote kwa mafunzo yote ada yake haizidi shilingi 120,000 kwa bweni na 60,000/=kwa wanafunzi wa kutwa na gharama nyingine zinawezeshwa na Serikali.
Naye Kaimu Msajili VETA Chang'ombe, Ziada Shekimweri amesema wanaohitaji kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi ni wengi na pia ameipongeza serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu mbalimbali yakiwemo madarasa na ujenzi wa vyuo vya VETA kwa kila Wilaya.
Kwa upande wa Mwanafunzi Rafaeli Mmanyi ambaye yuko mwaka wa pili katika fani ya The Toyota Hybrid System mfumo ambao unatumia vitu viwili yaani injini na mota kwa ajili ya magari ameishukuru serikali kwa udhamini wanaotoa kuwadhamini wanafunzi katika fani mbalimbali
Mwalimu wa Eletronic, Ricky Sambo akizungumzia fani mbalimbali zinazotolewa na vyuo vya VETA Kanda ya Dar es Salaam.Kaimu Msajili VETA Chang'ombe, Ziada Shekimweri akizungumzia mafanikio kadhaa ya VETA.
Mwanafunzi Rafaeli Mmanyi ambaye yuko mwaka wa pili katika fani ya The Toyota Hybrid System akizungumzia namna ya mfumo huo unavyofanya kazi.
Mwanafunzi Mtaalamu wa maabara akielezea dawa mbalimbali ambazo VETA imezitengenezwa kwa ajili ya kazi mbalimbali.
Mwanafunzi wa masuala ya Printing, Dismas Musa akizungumzia kuhusu masomo ya fani hiyo.
Mwanafunzi Mfungo Changala akizungumzia kuhusu fani ya Mechatronics.
Mwanafunzi Daud Azaria akizungumzia somo la ICT.
Mwalimu Baraka Mwaikaje akizungumzia mafunzo ya utengenezaji wa simu. Kushoto kwake ni mwanafunzi wake wa fani hiyo ya fundi simu Amina Alphayo akiendelea na mafunzo kwa vitendo.
Mwanafunzi wa fani ya fundi simu Amina Alphayo akiendelea na mafunzo kwa vitendo.
Mwanafunzi wa fani ya uchoraji wa ramani na usanifu majengo, Deogratius John akielezea umuhimu wa fani hiyo.
Mwanafunzi wa fani ya ufundi bomba Gato Ngonyani akielezea matumizi mbalimbali ya vifaa vya bomba.
Mwanafunzi wa fani ya ufundi Selemara, Angel Mushi akionesha kiti ambacho unaweza kukitumia kama kiti na meza ambacho kinatengenezwa na VETA.
Wanafunzi wakionesha kifaa cha kukaushia mboga za majani jinsi kinavyofanya kazi. Kushoto ni Lea Grifin na Asha Iddy.
Walimu wa fani ya uchomeleaji wa vyuma kutoka kundi la watu wenye uhitaji wakionesha namna ya kifaa cha uchomeleaji jinsi kinavyofanya kazi.
Mwanafunzi wa fani ya ushonaji, Witness Kapinga (kushoto) akielekeza namna ya ushonaji wa mavazi mbalimbali. Kulia ni Mwalimu wa fani hiyo, Theresia Anthony.
Mwalimu wa fani hiyo, Theresia Anthony. akionesha moja ya nguo iliyoshonwa na wanafunzi wa VETA.
Mashine ya ukataji wa vyuma inayotengenezwa na VETA ikioneshwa.
Wanafunzi wa VETA, Onesmo Paul na Zaituni Salum wakionesha kifaa cha usalama wa nyumba yako ambacho kinawasha taa au kupiga aram iwapo dirisha lilofungwa kifaa hicho kama mtu atakuwa ameligusa.Mwalimu wa fani ya utengenezaji wa mashine ya kukatia chumo, Emmanuel Bukuku, akizungumzia umuhiu wa kifaa hicho na jinsi kinavyorahisisha kazi kwa mtumiaji.
No comments