Breaking News

TCRA YAVITAKA VYOMBO VYA HABARI KURIPOTI UCHAGUZI MKUU 2025 BILA YA UPENDELEO

Meneja wa Kitengo cha Utangazaji TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo Machi 15, 2025.

.................................................

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imevitaka vyombo vya habari nchini katika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu kuvipatia vyama vya siasa nafasi sawa katika kuripotiwa habari bila upendeleo ili kuondoa malalamiko.

Meneja wa Kitengo cha Utangazaji TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka ameyasema haya leo katika Mkutano wa Misa Tanzania na Wadau (MISA-TAN - Wadau Summit 2025) uliofanyika jijini Dodoma, Mhandisi Kisaka amesisitiza umuhimu wa vyombo vya habari kufanya kazi kwa usawa, haki na uadilifu, hasa wakati wa kuripoti habari za vyama vya siasa.

Amesema, kuvipatia haki sawa vyama vya siasa itasaidia kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa sahihi na zinazowawezesha kufanya uamuzi wa busara hususani wa kuchagua viongozi wanaowataka na sio kukipatia chama kimoja muda mrefu wa kujieleza na kuvinyima vingine, kwani ni kosa kisheria na hatua za kinidhani zitachukuliwa.

No comments