MKE WA RAIS WA FINLAND ATEMBELEA MAKUMBUSHO
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii ,Dkt Hassan Abbas (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mke wa Rais wa Finland allipotembelea makumbusho ya taifa ili kujionea vivutio mbalimbali na utamaduni wa mali kale‎ Jijini Dar es Salaam Mei 14, 2025. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Makumbusho ya Taifa ,Dkt Noel Lwoga.
...................................................
‎Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam‎
‎
‎KATIBU Mkuu Wizara ya Mali Asili na Utalii ,Dkt Hassan Abbas amesema Tanzania na Finland wamekuwa na mashirikiano mazuri kwa muda mrefu katika sekta ya misitu ikihusisha masuala ya utafiti na kubadilishana wataalam katika sekta ya misitu na kuiongezea uwezo nchi juu ya uwezeshaji katika eneo la utalii. ‎
‎
‎Hayo yameelezwa leo Mei 14, 2025 Jijini Dar es Salaam na Katibu huyo wakati wa mke wa Rais wa Finland allipotembelea makumbusho ya taifa ili kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo pamoja na utamaduni wa mali kale
‎
‎Hii ni sehemu ya ziara fupi ya Rais wa Finland kutembelea nchi ya Tanzania pia katika ziara hiyo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan atazindua mradi wa dola Pound milioni 20 sawa shilingi milioni 40 za Kitanzania ambapo huu ni mradi mpya utakaosaidia kukuza na kuendeleza sekta ya misitu.
‎
‎Nchi yetu imekua na mashirikiano mazuri na nchi ya Finland kwahiyo sisi ni marafiki wa muda mrefu ambapo hata Rais Hayati Mwalimu Julius Nyerere alitembelea nchini Finland mwaka 1973.
‎
‎"Sisi wizara ya mali asili na utalii tunanufaika sana na wenzetu wa Finland hasa katika sekta ya misitu, tuna ushirikiano wa zaidi ya miaka 40, miradi ambayo tumekuwa tukiifanya inayohusu misitu na mazao yake, huu mradi ambao tutausaini kesho kutwa ni muendelezo wa haya yote ambayo wamekuwa wakitusidia"alisema Katibu Mkuu Abbas
‎
‎Naye Mkurugenzi Mkuu Makumbusho ya Taifa ,Dkt Noel Lwoga amesema ujio wa mke wa Rais kutoka Finland ni mafanikio makubwa ya Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuutangaza utalii pia ni alama kwa Wizara ya mali asili na utalii katika kupanua wigo wa kutangaza vivutio vya utalii nchini.
‎
‎Aidha amesema kuwa makumbusho ya Taifa wanashughulika na tafiti ,ukusanyaji, uendelezaji na kutoa elimu kwa Jamii, hivyo wangependa kushirikiana na nchi ya Finland katika kufanya utafifi katika eneo la tamaduni na mali kale kwani nchi ya Finland wao wamepiga hatua katika eneo hilo kwa kiasi kikubwa
‎
‎Hata hivyo Mkurugenzi Lwoga ametoa hamasa kwa watanzania na wageni waendelee kutembelea makumbusho ya taifa kwa ajili ya kujifunza historia ya taifa, utamaduni na urithi pamoja kufahamu muingiliano wa nchi ,mataifa mengine na mashirikiano mazuri baina ya nchi na mataifa mengine.
Mkurugenzi Mkuu Makumbusho ya Taifa ,Dkt Noel Lwoga akizungumza na wanahabari kuhusu ziara hiyo. |
Post Comment
No comments