TAMISA WAMSHUKURU RAIS KUIFUNGUA SEKTA YA MADINI

Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano Tanzania (TAMISA) ,Dkt.Sebastian Ndege  akizungumza na  na Waandishi wa Habari kuhusu Kongamano litakalofanyika Mei, 26, 2925 Jijini Dar es Salaam.‎

......................................

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam‎

‎TAASISI ya Usambazaji Sekta ya Madini Tanzania (TAMISA) wamemshukuru Rais wa Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuifungua sekta ya madini katika soko la kimataifa na kuweka mikakati ya kuhakikisha wazawa wanapiga hatua katika sekta hiyo hapa nchini.‎

‎Kauli hiyo imetolewa Leo Mei 14,2025 Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano TAMISA,Dkt.Sebastian Ndege  wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Kongamano litakalofanyika Mei, 26 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.‎

‎Dkt.Ndege amesema kwamba wafanyabiashara wazawa paamoja wadau  katika sekta ya madini na Chama Cha Wachimbaji Wadogo  wa Madini wametakiwa kujiunga na  TAMISA kwa lengo la kuwa na sauti moja katika kufikia malengo.‎

‎Aidha ,amesema kwamba katika kongamano Hilo litajadili  changamoto na namna ya kuzifikia fursa zilizoko kwenye sekta ya madini na kuzindua Kamati ya Mawasiliano.‎

‎Pia ameeleza kwamba mgeni rasmi wa kongamano Hilo ni Waziri wa Madini Antony Mavunde ambapo itakua ni siku rasmi ya kuzindua Kamati ya Mwasiliano ambayo italuwa na jukumu la kuhabarisha umma na wadau wa sekta ya madinu juuya fursa zinazopataikana katika sekta ya madini kupitia  website.‎

‎Kwa upande wake  Mwenyekiti wa TAMISA, Peter Kumalilwa amesema kwamba katika uongozi  wake amejipanga  kuhakikisha  kunakuwepo na  viwanda  vya wazawa vinavyohusiana na madini na kuhakikisha shilingi trillioni 3.1 zinazotolewa na kampuni kubwa za madini hapa nchini wazawa wachangie zaidi ya asilimia 20 au zaidi jambo ambalo watakuwa wakijivunia kama Watanzania.‎

‎Amemalizia kwa kusema kwamba TAMISA ina  majukumu ya kuhamasisha wazawa kufungua vyama vya  madini, kuhabarisha wadau  mbalimbali kuhusu fursa zinazopatikana kupitia sekta hiyo  na kuwaunganisha wadau wazawa kuwa sauti moja ili kufikia mafanikio yanayohitajika.

‎Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano Taasisi ya Usambazaji Sekta ya Madini Tanzania ( TAMISA),Dkt.Sebastian Ndege  akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Mei 14,20225 Jijini Dar es Salaam kuhusu Kongamano litakalofanyika Mei, 26 mwaka huu Jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi wa kongamano hilo anatarajiwa kuwa Waziri wa Madini Antony Mavunde.

No comments