ALEX MSAMA: WATANZANIA PUUZENI TAARIFA ZINAZODAI NIMEFUKUZWA KWENYE NYUMBA YANGU UPANGA
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama
...............................
Na Dotto Mwaibale
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama amewataka watanzania kupuuza habari zinazozagaa ambazo zinadai kuwa amefukuzwa kwenye nyumba yake iliyopo eneo la Upanga Jijini Dar es Salaam.Msama amesema taarifa hizo zimelenga kumchafua hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
"Video zinazosambaa zinatumika na watu wasio na nia njema na mimi na wana lengo la kunichafua hasa kipindi hichi cha vita za ubunge,” amesema Msama.
No comments