DAS WILAYA YA BUKOBA AONGOZA UKAGUZI WA ENEO LILILOVAMIWA TARAFA YA KATERERO

Ahimiza kulinda maeneo ya vijiji kwa manufaa ya wote.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukoba (DAS) Bi. Proscovia Mwambi (mwenye koti la njano) akikagua eneo ambalo lilikuwa limevamiwa na wananchi Kijiji cha Kyema katika Tarfa ya Katerero wakati wa ziara aliyoifanya Juni 11, 2025. Kulia kwake ni Afisa Tarafa hiyo, Bwanku M Bwanku na Polisi Kata Kemondo Afande Hakika Pastory.

...................................

Na Mwandishi Wetu, Bukoba

KATIBU Tawala wa Wilaya ya Bukoba (DAS) Bi. Proscovia Mwambi Leo Jumatano Juni 11, 2025 amefanya ziara kwenye Tarafa ya Katerero akiongozana na Afisa Tarafa hiyo, Bwanku M Bwanku, Mtendaji wa Kata Bi. Sophia Busunge, Polisi Kata Kemondo Afande Hakika Pastory na Viongozi wengine wa kijiji kukagua eneo la Kijiji cha Kyema lililopo Kitongoji cha Kyanjojwe lililovamiwa na baadhi ya wananchi na kulitumia bila utaratibu.

DAS Mwambi alikagua eneo hilo na kuwaeleza Viongozi na Wananchi kuhakikisha wanalinda maeneo yote ya vijiji na kuhakikisha yanatumika kwa utaratibu badala ya kuvamiwa au kuuzwa kinyemela kwa manufaa binafsi ya wachache huku akiwahakikishia wananchi kwamba Serikali ya Wilaya ya Bukoba haitakubali kuona wananchi wananyanyaswa kwenye maeneo yao.

Kumekua na wimbi la ardhi za vijiji kuvamiwa ama kuuzwa na Viongozi na Wananchi bila kufuata jambo lililoamsha Uongozi wa Wilaya kwa kushirikiana na Tarafa na Kata kuweka mikakati kabambe kudhibiti uvamizi na uuzwaji wa ardhi za Vijiji ili kulinda ardhi hizo kwa manufaa ya wengi na si wachache.

Ukaguzi wa eneo hilo ukiendelea
Viongozi wa tarafa hiyo wakiwa katika eneo hilo lililovamiwa.
 

No comments