MWENYEKITI TADEA DKT. PROSPER MAGALI ATAJA MAFANIKIO WIKI YA NISHATI JADIDIFU 2025
..............................................
Na Angelina Mganga, Dar es Salaam
‎MWENYEKITI wa Jumuiya ya Nishati Jadidifu Tanzania, Dkt.Prosper Magali(TADEA) amesema kwamba wamekuwa na mafanikio mengi yaliyopatikana katika wiki ya Nishati Jadidifu kwa mwaka huu 2025.‎
‎Dkt.Magali amebainisha mafanikio hayo wakati wa mahojiano maalum yaliyofanyika kwa njia ya simu na mwandishi kwa kueleza kwamba jumla ya washiriki 300 pamoja na makampuni 23 walishiriki.‎
‎Makampuni hayo yaliweza kuonesha bidhaa mbalimbali katika Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Mwezi Mei.‎
‎Ameeleza kwamba katika mkutano huo waliweza kufanya majadiliano mbalimbali kutoka kwa wadau waliohudhuria na kupata ufunguzi wa changamoato mbalimbali.‎
‎Sambamba na hayo wananchi walipata fursa yakujionea bidhaa mbalimbali na kupata elimu yakutumia nishati mbadala waliotembelea mabanda ya maonesho hasa nishati safi ya kupikia.‎
‎Dkt.Magali ameishukuru serikali kwa ushirikiano wanaowapatia sekta binafsi kwa kuweka mazingira mazuri na wezeshi na kuhakikisha sekta binafsi kufanya kazi zake vizuri na kutambua umuhimu wa sekta binafsi hasa katika kipindi hiki chakuhamasisha matumizi ya nishati safi yakupikia.‎
‎Hata hivyo amesema mpango mkakati wa Taifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ni kutoa elimu kwa wananchi kwa ngazi zote hasa vijijini kwa Tanzania nzima ili kuhifadhi mazingira na kulinda afya kwa kutumia nishati safi ya kupikia.‎
‎Sanjari na hayo ameeleza changamoto ya ufahamu na uelewa kwa baadhi ya maeneo kwa hiyo watajitahidi kutoa elimu na jinsi yakutumia majiko banifu,mkaa mbadala pamoja na majiko yanayotumia umeme.‎
‎Ameendelea kwa kueleza kwamba changamoto ya upatikanaji ya mitaji limekua ni jambo ambalo fedha zinapatikana kwa masharti hivyo wanaiomba serikali kuliangalia jambo hili kwa jicho lakipekee.‎
‎Amesema kwamba makusudi ya Serikali kuhakikisha vifaa vinapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu.‎
‎Wiki ya nishati jadidifu ilifanyika Mei 26 na kuhitimishwa Mei 29,2025 Jijini Dar es Salaam ‎
‎Dhamira ya Serikali ni kuongeza uzalishaji wa umeme Jadidifu katika maeneo mengi ili kufikia malengo ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ifikapo 2030.
Post Comment
No comments