POLOKANYA -ALMASI ILIYOFICHIKA KATIKA MTO WAMI ULIOPO HIFADHI YA TAIFA SAADANI
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Saadani, , Gladys Z. Ng'umbi
............................................
Mashaka Kibaya,Tanga.
KATIKA ukanda wa kaskazini mashariki mwa Tanzania, palipojificha historia, uzuri wa asili, na simulizi ya kuvutia, ndipo ilipo Polokanya, sehemu ya kipekee iliyo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani.
Mahali hapa ni hazina ya Ikolojia, na zaidi ni lango la ajabu ambapo mto hukutana na bahari – Mto Wami unamwaga maji yake moja kwa moja katika Bahari ya Hindi, hali ambayo ni ya kipekee kabisa nchini Tanzania.
Nimefanya mahojiano maalum na Askari wa Wanyamapori Daraja III, Poroto Japhari, naye akafungua ukurasa wa historia na kuvutia kwa eneo hili:
“Karibuni sana Mto Wami, kwenye kituo cha Polokanya. Zamani kabla ya hapa kuwa hifadhi, kulikuwa na raia mmoja wa kiasia.
Hifadhi ya Kipekee Inayokumbatia Bahari na Nyika\
Katika ukanda wa Afrika Mashariki, kuna hifadhi moja tu ya taifa inayokutana na bahari moja kwa moja — Hifadhi ya Taifa ya Saadani. Hifadhi hii si tu kipekee kijiografia bali pia kimazingira na kiutalii.
Iko katika mikoa ya Pwani na Tanga, na tangu kuanzishwa mwaka 2005 kupitia Tangazo la Serikali Na. 281, imeendelea kuvutia wageni wa kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Katika mahojiano maalum na Naibu Kamishna wa Uhifadhi (Assistant Conservation Commissioner), ambaye pia ni Kamanda wa Hifadhi ya Saadani, Gladys Z. Ng'umbi, ameeleza kwa kina mafanikio na nafasi ya kipekee ya hifadhi hii miongoni mwa hifadhi 21 za taifa nchini Tanzania.
“Saadani ni ya kipekee kwa kuwa ni hifadhi pekee ukanda huu wa Afrika Mashariki inayokutana moja kwa moja na bahari. Hii inaleta mvuto mkubwa kwa ikolojia na utalii,” amesema Gladys.
Mazingira Anuwai Yenye Mifumo Tofauti ya Ikolojia
Hifadhi hii ina mandhari ya kuvutia ikijumuisha bahari, Mto Wami, misitu ya Zaraninge, maeneo ya savanna, na mifumo ya baharini maarufu kama marine ecosystem.
Katika maeneo haya, wanapatikana wanyama wa aina mbalimbali, ndege wahamiaji kutoka mabara tofauti, na viumbe wa baharini kama kasa, hupatikana.
Gladys ameeleza kuwa juhudi za Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zimesaidia sana kukuza utalii katika Saadani kupitia filamu maarufu ya Royal Tour, ambayo imesaidia kuitangaza Tanzania kimataifa.
Vivutio na Shughuli za Utalii
Watalii wanaweza kushiriki katika shughuli nyingi za kipekee kama vile:
Boat safaris katika Mto Wami hadi eneo maalum la "eco-zone" ambapo mto hukutana na bahari.
Game drive mchana na hata usiku kwa lengo la kuwaona wanyamapori.
Kutembelea kituo cha kihistoria cha Caravan kinachosimamiwa pia na hifadhi.
Wanyamapori wanaopatikana ni wengi wakiwemo wanyama wakubwa maarufu kama “Big Five” – Simba, Chui, Tembo, Nyati, na faru ambaye bado hajapatikana Saadani kwa sasa.
Aidha, kuna wanyama wengine kama pongo, twiga, swala, pundamilia, fisi, na aina nyingi za ndege wahamiaji.
Idadi ya Watalii na Fursa za Uwekezaji
Kwa mwaka wa fedha 2024/2025 hadi sasa, watalii wa kimataifa ni 8,245 huku wa ndani wakiwa 19,124. Idadi hii inathibitisha ongezeko la watalii na mchango wa sekta hii katika uchumi wa nchi.
Gladys pia ametaja fursa zilizopo katika hifadhi hiyo ikiwa ni pamoja na:
Uwekezaji kwenye malazi ya kitalii kama vile lodge, bandas, hosteli, maeneo ya kupiga kambi na “special campsites”.
Ujenzi wa permanent tented camps kwa mujibu wa taratibu za TANAPA.
Maendeleo ya miundombinu ikiwemo barabara, ambazo licha ya changamoto nyakati za mvua, serikali inaendelea kuziboresha kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.
Usalama na Ushirikiano na Wananchi
Ulinzi umeimarishwa kwa kushirikisha askari wa hifadhi na wananchi wanaoishi pembezoni mwa hifadhi, ambao hushiriki katika doria za mara kwa mara ili kudhibiti ujangili na kuhifadhi rasilimali.
Njia za kufika Saadani ni nyingi — kwa anga, reli, na barabara huku mchakato ukiwa unaendelea kuwezesha usafiri wa boti kutoka Zanzibar, hatua inayolenga kurahisisha ufikaji wa wageni hasa wa kimataifa.
Mwitikio wa Watanzania Kuhifadhi Mazingira
Viumbe kama kasa, walioko hatarini kutoweka, ni sehemu ya urithi muhimu unaolindwa Saadani. Gladys ametoa wito kwa Watanzania kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia katika kutangaza utalii wa ndani, kuhifadhi mazingira na kuhakikisha maliasili zinakuwa endelevu kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Saadani si tu kivutio, bali ni darasa la moja kwa moja kuhusu muunganiko wa mazingira ya bahari na bara – mali ya kipekee kwa Tanzania na Afrika
Askari daraja la tatu, Poroto Japhari.
Viboko hao wapo Mto Wami..
Ndege wakiwa juu ya mitiya hifadhi hiyo
Muonekano wa mto Wami
Muonekano wa maeneo yenye mandhari nzuri kwenye hifadhi hiyo
No comments